RAIS LUNGU AKIWA KANISANI
RAIS Edgar Lungu  ameelezea kusikitishwa kwake na ajali ya basi iliyoua watu 17 kwa mpigo, iliyotokea Luangwa jana.
Alisema yeye akiwa kama kiongozi wa taifa hilo amekumbwa na majonzi sana kutokana na ajali na kuwataka watumiaji wa barabara kufuata sheria ili kuepusha ajali zinazomaliza watu na mali.
“ Nimesikitishwa sana na vifo vya watu kumi na saba kufuatia ajali ya gari huko Luangwa  Mei 23, 2017.
Ajali ya basi hilo la Kapena lililokuwa linaelekea Chipata, jimbo la Eastern ilitokea baada ya dereva kushindwa kumudu basi katika kona.
Lungu pia aliwatumia ndugu jamaa na marafiki wa waliopoteza maisha na kuwataka kuwa na subira.
Rais Lungu aliwataka wananchi, watumiaji wa barabara na mamlaka husika kuhakikisha sheria zinafuatwa ili kupunguza ajali.


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO