MMOJA wa familia ya kifalme ya Japan,Princess Mako ameamua kuolewa na mtu wa kawiada katika nchi hiyo na hivyo kuachana na marupuru ya kuwa mmoja wa familia ya kifalme.
Binti huyo mwenye umri wa miaka 25 mjukuu mkubwa wa Mfalme Akihito ataolewa na Kei Komuro, ambaye pia ana miaka 25 na mfanyakazi wa kampuni ya uwakili.
Wawili hao walikutana chuoni.
Sheria za kifalme zinamtaka anayeolewa kuondoka katika himaya ya kifalme.
Mjukuu huyo anaolewa kwa mtindo huo wakati babu yake akitangaza kwamba anataka kuachia ufalme kutokana na kupanda kwa umri.
Mako na Kei Komuro walikutana mwaka 2012 katika mgahawa mmoja wakati wanasoma  Chuo kikuu cha International Christian mjini Tokyo.
Ndoa hiyo inatarajiwa kufungwa mwakani
mwisho

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO