KABUL, Afghanistan
Watu 80 wamekufa na wengine mamia kujeruhiwa katika shambulio la mambomu yaliyojazwa mabomu nchini Afghanistan karibu na makazi ya Rais.
Imeelezwa kuwa idadi ya watu waliokufa itazidi kuongezeka kwani majeruhi wengi walikuwa katika hali mbaya.
Hili ni shambulio kubwa na baya la aina zake.
Shambulio hilo kubwa limetokea karibu na skwea ya Zanbaq ambayo ndiyo inayofikisha katika ofisi ya Rais.
Mkuu wa Polisi wa Kabul, Jenerali Hassan Shah Frogh,  alisema kwamba mlipuko uliotyumika ulikuwa umewekwa katika gari la majitaka.
Aidha mlipuko ulikuwa mkubwa kiasi ya kwamba uliacha shimo la mita nne.
Msemaji wa  Wizara ya afya Wahidullah Majrooh, amesema watu 80 wamekufa na 350 wamejeruhiwa.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO