Dr. Ntuyabaliwe Foundation yahimiza wanafunzi kusoma vitabu

Wananafunzi wa Shule za Msingi jijini Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla, wametakiwa kujenga utamaduni wa kupenda kusoma vitabu vikiwemo v...

Wananafunzi wa Shule za Msingi jijini Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla, wametakiwa kujenga utamaduni wa kupenda kusoma vitabu vikiwemo vya kiada na ziada, ili waweze kupanua wigo wa uelewa wa mambo mbalimbali. Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi, alipozungumza na wanafunzi, walimu na wajumbe ya Kamati ya Shule ya Msingi Makumbusho, wakati akizindua maktaba iliyokarabatiwa na mfuko huo. Amesema upo umuhimu mkubwa kwa wanafunzi kusoma vitabu vya kielimu, historia na pia hadithi. [caption id="attachment_1983" align="aligncenter" width="1404"] Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo la maktaba katika shule ya msingi Makumbusho jana jijini Dar es Salaam.(Picha zote na thebeauty.co.tz)[/caption] Awali Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo, alitoa shukrani kwa Dr. Ntuyabaliwe Foundation kwa mchango wake wa vitabu kwa ajili ya maktaba hiyo, na kuomba kupatiwa mtaalam wa kutunza maktaba, ikiwezekana mwalimu mmoja akasomeshwe taaluma hiyo. Naye Afisa Taaluma Fatma Mwiru akimwakilisha Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni, amewataka waalimu kuwasaidia wanafunzi kupata vitabu mbalimbali, kwa kuwashirikisha wadau wa elimu, wachapishaji vitabu pamoja na wahisani. [caption id="attachment_1984" align="aligncenter" width="1404"] Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo akizungumza alipokuwa akimkaribisha Mama Jacqueline Mengi.[/caption] Aidha Mama Jaqueline Mengi amesema Dr. Ntuyabaliwe Foundation ilianzishwa mwaka jana ikiwa na lengo la kuchangia katika sekta ya elimu, ambapo iligundua shule nyingi za msingi zinakabiliwa na uhaba wa maktaba na vitabu. Shule ya Msingi Makumbusho inakuwa ya shule ya pili katika wilaya ya Kinondoni na ya kwanza katika kata ya Makumbusho, kusaidiwa ujenzi wa maktaba na msaada wa vitabu na Dr. Ntuyabaliwe Foundation, ikitanguliwa na Shule ya Msingi Hananasifu. [caption id="attachment_1985" align="aligncenter" width="1404"] Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi alipowasili katika shule ya msingi Makumbusho jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_1986" align="aligncenter" width="1404"] Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo akimkaribisha ofisini kwake Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi. Katikati ni Afisa Taaluma Fatuma Mwiru aliyemwakilisha Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni katika uzinduzi huo.[/caption] [caption id="attachment_1987" align="aligncenter" width="1404"] Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi akibadilishana mawazo na Afisa Taaluma Fatuma Mwiru aliyekwamilisha Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni.[/caption] [caption id="attachment_1989" align="aligncenter" width="1404"] Picha juu na chini ni Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi akizungumza na wanafunzi wa shule msingi Makumbusho kabla ya uzinduzi huo.[/caption] [caption id="attachment_1988" align="aligncenter" width="1404"] Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo akimwongoza Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi kuelekea eneo la uzinduzi wa maktaba hiyo.[/caption] [caption id="attachment_1991" align="aligncenter" width="1404"] Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi pamoja na Afisa Taaluma Fatuma Mwiru, aliyemwakilisha Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la maktaba hiyo.[/caption] [caption id="attachment_1992" align="aligncenter" width="1404"] Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi akisoma moja ya vitabu vya hadithi kwa baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Makumbusho waliowakilisha wenzao katika uzinduzi huo.[/caption] [caption id="attachment_1993" align="aligncenter" width="1404"] Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi na Afisa Taaluma Fatuma Mwiru, aliyemwakilisha Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni kwa pamoja wakizundua rasmi eneo la kuhifadhia vitabu ndani ya maktaba hiyo.[/caption] [caption id="attachment_2006" align="aligncenter" width="1404"] Baadhi ya wageni waalikwa akiwemo Miss Tanzania 2008 Nasreen Karim (wa pili kulia).[/caption] [caption id="attachment_1995" align="aligncenter" width="1404"] Baadhi ya watoto wa shule ya msingi Makumbusho wakisoma vitabu mbalimbali vilivyotolewa msaada na Dr. Ntuyabaliwe Foundation.[/caption] [caption id="attachment_1997" align="aligncenter" width="1404"] Picha juu na chini ni Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi pamoja na walimu na wajumbe wa kamati ya shule wakikagua vitabu katika maktaba hiyo.[/caption] [caption id="attachment_2000" align="aligncenter" width="1404"] Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi katika picha na walimu pamoja na wajumbe wa kamati shule.[/caption] [caption id="attachment_2001" align="aligncenter" width="1404"] Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi waliowakilisha wenzao.[/caption] [caption id="attachment_2004" align="aligncenter" width="1404"] Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi katika picha ya pamoja na walimu na wajumbe wa kamati ya shule.[/caption] [caption id="attachment_2002" align="aligncenter" width="1404"] Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Bernadicta Lyimo (katikati) akionyesha waandishi wa habari na wageni waalikwa (hawapo pichani) muonekano wa awali kabla ya jengo hilo kukarabatiwa Dr. Ntuyabaliwe Foundation. Kushoto ni Mama Mengi na kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Shule, Haji Shabani Kibwana.[/caption] [caption id="attachment_2005" align="aligncenter" width="1404"] Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi akifurahi na kuimba na wanafunzi wa shule ya msingi Makumbusho baada ya kukamilika kwa shughuli ya uzinduzi wa maktaba shuleni hapo.[/caption]  

COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,302,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4816,habari. dodoma,24,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: Dr. Ntuyabaliwe Foundation yahimiza wanafunzi kusoma vitabu
Dr. Ntuyabaliwe Foundation yahimiza wanafunzi kusoma vitabu
http://www.thebeauty.co.tz/wp-content/uploads/2017/05/GV1A9520.jpg
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2017/05/dr-ntuyabaliwe-foundation-yahimiza.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2017/05/dr-ntuyabaliwe-foundation-yahimiza.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy