HIVI ni katika umri gani baba na mama watakuwa wamepata nafuu ya kuacha kulazimika kuhudumia watoto wao?
Hilo ni swali lakini Jaji mmoja kaskazini mwa Hispania amekataa ombi la mdada mmoja mwenye umri wa miaka 23 kuendelea kusaidiwa na wazazi wake na kumwambia kwamba alikuwa mvivu mno kuweza kuendelea kusaidiwa.
Pamoja na ukweli kuwa Hispania ambayo watoto huendelea kusaidiwa hadi wanapofikisha miaka 30, wazazi wengi wamekuwa wakitafuta msaada wa kisheria kuondokana na mzigo huo kutokana na hali ya kiuchumi na pia kukabiliana na vijana ambao ni wavivu wa kujitafutia shughuli za kufanya.
Kutokana na kupromoka kwa uchumi wa Hispania vijana wengi wamekosa kazi an kuwa tegemezi kwa wazazi wao.
Mdada huyo wa miaka 23  wa Castro Urdiales, alienda kuwashtaki wazazi wake katika mahakama ya mkoa ya Cantabrian  akitaka apewe matumizi ya euro 300 kila mwezi kutoka kwa baba yake.
Imeelezwa kuwa wazazu wa mtoto huyo waliachana mwaka 2012 lakini katika makubaliano yao hapakuwepo na suala la kutunza watoto.
Hata hivyo mahakama iliambiwa kwamba binit huyo hakufanikiwakumaliza masomo ya sekondari lakini pamoja na kupewa fedha za kujifunza Tehama kutoka kwa wazazi wake kozi hizo pia hakumaliza.
Sheria inataka wazazi kusaidia mtoto mpaka ajitegemee lakini majaji wamesema kwamba wajibu hauwezi kuwa lazima kama  tabia za mtoto hazioneshi nia yake ya kujitegemea.
Mdada huyo aliambiwa hawezi kuendelea kupewa zawadi bila wajibu kwani yeye ni mvivu  asiyeweza kutumia fursa aliyopewa.
MKutokana na maamuzi hayo ya mahakama ya Catalonia kijana huyo alilazimikamkuondoka katika makazi ya wazazi wake.
Rais wa Shirikisho la sheria za kifamilia Maria Dolores Lozano, amesema wazazi wengi wamekuwa wakitafuta msaada wa kisheria kuondokana na watoto wasiofanya juhudi za kuachana na wazazi wao katika masuala ya kiuchumi na utegemezi.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO