SERIKALI mkoani Kigoma  katika kukabiliana na tishio la ugonjwa wa ebola ambao umetokea katika nchi jirani ya Kongo, imeimarisha udhibiti  mipakani,maeneo ya bandari na usafirishaji.

Aidha udhibiti unafanyika maeneo ambayo wakimbizi kutoka Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wanapokelewa wanapoingia nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Mganga Mkuu wa mkoa Kigoma Dk.Paul Chaote(pichani).

Aidha amesema kwamba timu za usimamizi na utekelezaji wa jambo hilo zimeshakutana na kuangalia nini cha kufanya .

Aidha  manispaa ya Kigoma Ujijini imeshachagua eneo kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wa Ebola iwapo itagundulika kuna mtu ameingia na ugonjwa na kwamba tahadhari kubwa imechukuliwa kuhakikisha hakuna mtu anayeingia nchini na ugonjwa huo bila kutambulika na mamlaka husika.


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO