POLISI Mkoani Morogoro linamshikilia Dereva wa Lori  Erasto Kingazi (33) mkazi wa Yombo, Dar es Salam  kwa tuhuma za kuendesha lori lakekizmbe na kugongana uso kwa uso na basi la abiria.

Basi hilo lilikuwa likitokea Turiani,  wilayani  Mvomero kwenda mjini Morogoro.

katika ajali hiyo watu 24 wamejeruhiwa na kukimbizwa  Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kupata matibabu.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei, alisema kuwa ajali hiyo ilitokea leo  Mei 7  majira ya saa sita mchana eneo la Ranchi Dakawa , kwenye  barabara kuu ya Dodoma – Morogoro , wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro.

Alisema  dereva wa Lori hilo lenye namba za usajili T 712 CHP na Tela lake namba T591 BYS aina ya Scania likiwa limebeba mzigo lilikuwa likielekea nchini Rwanda.

Alisema lilipofika eneo hilo dereva huyo alikuwa akiyapita magari mawili yaliyombele yake bila kuchukua tahadhari na kusababisha kugongana uso kwa uso na basi  lenye namba za ujasili T637 DGN aina ya Tata likiwa linatokea Turiani kwenda mjini Morogoro.


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO