Grand Hyatt Cannes Hotel Martinez


Kiota hiki kipo Boulevard de la Croisettekikitazamana na Ghuba ya Cannes. Kiota hiki Grand Hyatt Cannes Hotel Martinez  ndicho kilicho maarufu sana kwa watu wenye fedha zao  wanaotaka kupati mpaka asubuhi kwenye tamasha la filamu la  Cannes .

mwaka jan a Jake Gyllenhaal, Thierry Fremaux na Sienna Miller walionekana katika veranda ya hoteli hii maarufu. Bruce Willis, Robert Pattinson na Eva Longoria pia wamedaiwa kuishi katika hoteli hii wakati wa tamasha.

Hoteli hii inavyumba vya kifahari 409,pamoja na vyumba maalumu (suites) 27 iikiwa na Penthouse Suites kubwa barani Ulaya. Hoteli pia ina ufukwe binafsi mkubwa zaidi huko  Croisette  na wana zaidi ya 400 wanaojianika katika eneo hilo.


La Palme d'Or

Ikiwa karibu na Hotel Martinez, La Palme d'Or  ina Michelin Stars mbili na inafikirika kwamba ina mgahwa bora zaidi duniani kuutembelea ukiwa ndani ya boti ya kifahari ya hali ya juu zaidi. Ikiwa imetajwa kwa jina la tunzo za tamasha huwa inavcutia wageni wengi hasa kujipatia chakula cha usiku. Inajulikana wazi kwamba watu mashuhuri kama Sharon Stone na Elton John  wameshajipatia mlo katika magawa uliomo hotelini hapa.

Ikiwa imejengwa mwaka 1985 na Christian Willer, La Palme d'Or iliadhimisha miaka 30 ya uwapo wake mwaka jana kwa kumwezesha Sinicopri kuonesha makeke yake katika mlo wa kienyeji. Chayla  bomba ni pamoja na Spider .


Hotel du Cap Eden Roc
Ikiwa dakika 30 kutoka Cannes wageni wengi mashuhuri huchagua eneo hili lenye ufahari wa aina yake wakati wa tamasha la Cannes wageni wake ambaopw ameshapita hapa ni wale wa daraja A unaweza kusema kama akina Clint Eastwood, Sharon Stone, Jennifer Lopez, Colin Firth na Johnny Depp.

Cap Eden Roc  ina heshima ya kutembelewa na boti za kifahari za ngazi za juu kutokaa na kuwa na mazingira mazuri ya muono, bustani zinaztia kiwi, ukanda wa pwani ambao ni wa utawala binafsi na bwawa la kuogelea lisilokuwa na mwisho. Kiukweli hili ndilo eneo bomba zaidi la kukaa wakati wa tamasha la filamu.


Tetou
Tetou ni moja ya eneo ambalo watu mashuhuri hupenda kubarizi wakati wa tamasha la cannes. Mwaka jana Charlize Theron na Sean Penn walionwa wakiwa katika chakula cha usiku  cha wapendanao pekee huku Jake Gyllenhaal alifotolewa akiwa anafurahisa chakula cha usiku na marafiki zake.

Ni mgahawa bomba katika French Riviera  ambao huwa malipo yake ni  keshi na si kw anjia ya kadi.


Le Bâoli
Ni eneo la watu wakujidai kwa ajili ya chakula cha jioni na kusakata densi. mwaka jana Le Bâoli  lilikuwa n eneo walilokutana watu wa The Sea Of Trees  na miongoni waliokuwapo katika hafla hiyo ni pamoja na Naomi Watts, Sienna Miller na Camila Alves.
Klabu hii ni mashuhuri sana miongoni mwa watu wanaoheshimika sana nchini Ufaransa ikiwa na  vaibu ya hip hop na  electronica.

InterContinental Carlton Cannes
Ni eneo lenye kazi nyingi kama nyuki wanapotengeneza asali. Hoteli hii ambayo imejengwa mwaka 1911 ipoe Boulevard de La Croisette ikiangaliana na ghuba ya Cannes. Ina fukwe yake, mgahawa wa aina yake na pia hutoa aina fulani ya michezo ya katika maji.

Hoteli hii ina histori ya aina yake na mpaka leo kuna suite inayotambuliwa kama Grace kelly yule mdada aliyepata date yake ya kwanza Prince Rainier wakati wa tamasha la filamu la mwaka 1955 .

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO