WANUFAIKA na mradi wa wa Airtel Fursa uliolenga kuwianua wajasirimali vijana wamesema kwamba wamepata mafanikio makubwa katika awamu ya kwanza ya mradi huo. 
Wamesema kwamba pamoja na mafanikio yao, wameitaka kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayotekeleza mradi kuendelea kusaidia vijana kujinasua na uchumi mbovu ukiwamo umaskini wa fikira. 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es saalam , mmoja kati ya waliowezeshwa mwaka jana, Threria Maliatabu  mkazi wa Mbagala jijini Dar es Saalam amesema amekuza kipato na kupata mafanikio na kwamba amejenga nyumba yake binafsi ya vyumba vinne. 
Aidha baada ya msaada aliopewa ameweza kujinunulia shamba la eka 2 huku akiwaasa vijana wenzake nchini na wale wote waliowezeshwa na Airtel FURSA kuchangamkia fursa hizi pindi zinapotokea. 
Maliatabu ambaye anajishughulisha na biashara ya uchoraji wa picha za sanaa alisema:  “ najivunia sana kuwa mmoja kati ya vijana walioshikwa mkono na Airtel Fursa kwa sababu program hii imeweza kunitoa kutoka nilipokuwa hadi kufika kwenye haya mafanikio niliyo nayo leo.” 
Alisema kwa msaada huo ameboresha kiwango cha bidhaa zake kiasi ya kwamba  biashara anayofanya ili mwezesha kukunua shamba la eka 2 Mkuranga mkoa wa pwani. 
Hata hivyo Maliatabu alifafanua kuhusu changamoto za biashara ikiwemo masoko ya nje , usafiri wa kusambaza bidhaa zake huku akieleza kuwa baadhi ya changamoto hizi ameshaanza kuzishughulikia  na kuomba wadau mbalimbali kuweza kumsaidia. 
“Nimeweza kuongeza masoko yangu na kufikia masoko ya Zanzibar, Moshi , Arusha na Dar, na kwa sasa niko katika mchakato wa kupeleka bidhaa zangu nchini Sweden na Italia. Mipango hii ikikamilika kwakweli nitakuwa nimefurahi kufikia malengo yangu na naamini nitafanya vizuri zaidi na kukuza kipato changu zaidi.” Alisema na kutoa wito kwa vijana wenzake kujikita kwenye ujasiriamali badala ya kusubiri ajira ambazo zimekuwa ni changamoto. 
Naye, Meneja Huduma kwa Jamii,  wa kampuni ya Airtel,Hawa Bayumi alisema kampuni yake inafarijika na kujisikia fahari kuona program waliyoianzisha imeweza kuwainua vijana wajasiriamali wenye nia ya kukuza kipato na kufikia malengo yao. 
“Theresia Maliatabu ni mfano wa kuigwa, alipowezeshwa alijiongeza na kufanya kazi kwa juhudi kubwa na maarifa. Nawaasa vijana wajitume na kuchangamkia fursa kama hizi zinapojitokeza wazitumie vizuri ili kuleta tija kwenye maisha yao, familia zao na taifa kwa ujumla.” alisema.                                                                                                                                                                     
Theresia Maliatabu ni moja kati ya vijana waliochagulia kuwa kati ya wafanyabiashara wadogo wadogo watakaonufaika na mpango wa Airtel FURSA  na kupatiwa vitendea kazi zikiwemo , ubao wa kuchorea, vifaa vya kuchorea na kompyuta, mafunzo ya ujasiriamali na kutengenezewa kipindi maalumu cha Television kilichoonyesha safari yake katika biashara ambavyo vimemsaidia kukuza biashara yake. 
Airtel  kupitia mpango wake wa Airtel fursa imewezesha vijana takibribani 5000 kwa kuwapatia mafunzo ya ujasirimali na baadhi yao kupata vitendea kazi ili kuboresha biashara zao.

MwishoPost a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO