Muigizaji maarufu wa sinema za James Bond, Sir Roger Moore, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 89.

Roger Moore ambaye anajulikana kwa kasi yake ya utoaji wa bastola na raha ya sauti katika kuondoka kwenye utata katika sinema za 007 amefariki kwa ugonjwa wa kansa.

Kifo cha Muigizaji huyu maarufu ambaye alicheza sinema  takaribani saba za James Bond ikiwamo Live and Let Die na A View to a Kill kilithibitishwa na familia yake.

Taarifa katika twita iliyoandikwa na watoto wake ilisema: "Thank you Pops for being you, and being so very special to so many people." (aksante baba kwa kuwa wewe, na kwa kuwa muungwana  na mtu maalumu kwa watu wengi) "With the heaviest of hearts, we must share the awful news that our father, Sir Roger Moore, passed away today. We are all devastated," .(kwa majonzi makubwa tunawapa taarifa za kufariki kwa baba yetu, Sir Roger Moore leo.Tumefadhaika sana)

Roger Moore ambaye alifanya vyema katika sinema hizo kuliko mgangulizi wake Sean Connery amefariki akiwa nchini Uswis na kwamba maziko yake yatafanyika binafsi katika nchi ya Monaco kwa mujibu wa matakwa yake.

Watoto wake Deborah, Geoffrey na Christian wamesema kwamba walimzunguka baba yao  katika siku zake za mwisho kwa mapenzi ambayo hayawezi kupimika wala kuelezeka na kwamba mawazo yao yanageuka kwa mama yao Kristina katika kipindi hiki kigumu.

Pamoja na uigizaji  wa sinema za Bond , Moore pia anajulikana kwa tamthilia z atelevisheni alizoigiza katika miaka ya 1960 za The Persuaders na The Saint.

Filamu alizocheza Sir Roger ambaye pia kuanzia miaka ya 1990 alikuwa balozi wa UNICEF ni:
Live and Let Die (1973)
The Man with the Golden Gun (1974)
The Spy Who Loved Me (1977)
Moonraker (1979)
For Your Eyes Only (1981)
Octopussy (1983)
A View to a Kill (1985)
SourceBBC

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO