MWENYEKITI na mwanzilishi wa shirika la habari la Fox News, Roger Ailes  amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 77.
Taarifa kutoka kwa mke wake Elizabeth  imesema kwamba inasikitika kueleza kwamba mwanzilishi huyo ameaga dunia.
Ailes ambaye aliendesha shirika la Fox News kwa miongo miwili anatambulika kwa kubadili mfumo wa uchakataji wa habari.
Mwenyekiti huyo aliachia ngazi mwaka jana baada ya wafanyakazi wengi wa kike kulalamika kwamba anawanyanyasa kijinsia akiwataka kimapenzi.
Wakati akitangza kujiuzulu alisema kwamba anafanya hivyo kutoa nafasy ya damu mpya kwani yeye amekuwa kama kikwazo cha maendeleo.
Kabla ya kuingia FOX alikuwa mshauri kw amarais kadhaa wa Marekani akiwamo Richard Nixon  na George Bush  mkubwa.
Ailes alikuwa mwanzishili wa Fox News mwaka 1996. Shirika hili linamilikiwa na tajiri wa vyombo vya habari Rupert Murdoch kupitia 21st Century Fox.
Inaaminika baada ya kutoka katika kampuni hiyo inaaminika alikuwa akisaidia kumwandaa Donald Trump kwenye midahalo mbalimbali.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO