POLISI nchini Zambia wamevamia baa  na vilabu vya usiku 30 mjini hapa na kuwatia mabroni vijana 259 chini ya miaka 18 ambao hawaruhusiwi kunywa wala kuwapo katika maeneo hayo.

Shughuli hiyo ilifanyika jana kwa kushirikiano kati ya polisi na watuj wa jiji la Lusaka.

Nia imeelezwa kuwa ni kuzuia vijana hao kunywa na kuzuru vilabu vya usiku ambapo pia wanapata nafasi ya kufanya mapenzi haramu.

Msemaji wa jijiji la Lusaka, Brenda Katongola, amesema vijana hao wameanza kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kushiriki ulevi na mapenzi kabla ya wakati.

katika operesheni hiyo  baa 15 zilipokonywa leseni kwa kuruhusu vijana chini ya miaka 18 kuwapo katika eneo la baa. Aidha waliopitisha muda nao waliporwa leseni.

hakuna baa inayoruhsuiwa kuendelea kuwa wazi baada ya saa nne usiku.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO