Katibu Tawala wa Wilaya ya Lindi, Thomas Safari akizindua rasmi Kampeni ya Hedhi Salama kwa Wasichana iliyoandaliwa na Chama cha Tanzania Girl Guids (TGGA), ikiwa ni sehemu ya shamrashamra ya maadhimisho ya Siku ya Hedhi Duniani itakayofikia kilele Mei 28. Uzinduzi huo ulifanyika kwenye Uwanja wa Ilulu mjini Lindi leo. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa TGGA, Mkoa wa Lindi, Zuhura Mohamed na Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA-KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari Mkoa wa Lindi wakiingia kwa maandamano kwenye Uwanja wa Ilulu, wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo.

Na Richard Mwaikenda-Lindi
SERIKALI ya Mkoa wa Lindi imekubali ombi la Chama cha Tanzania Girl Guids (TGGA), kwa kila shule kutenga chumba kimoja kwa ajili ya kujistiri wasichana wakati wa hedhi.

Ombi hilo lilitolewa na Katibu Mkuu wa TGGA Taifa, Grace Shaba wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Ilulu, mjini Lindi, ambapo aliiomba serikali na walimu wakuu wa shule kutenga vyumba mashuleni vya wasichana kujihifadhi wakati hedhi.

Shaba ambaye ni mwalimu mstaafu, alisema kuwa wakati akitumikia ualimu katika shule mbalimbali alikuwa anatenga vyumba kwa ajili ya kazi hiyo na kwamba viliwasaidia sana wanafunzi wasichana.

Akihutubia wakati wa hafla hiyo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Lindi, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya, Thomas Safari alisema vyumba vya siri kwa ajili ya wasichana wakati wa hedhi ni muhimu sana kwani vinawafanya wawe salama kiafya na wasafi wakati wote.

Alisema watahakikisha kwa kila shule katika mkoa huo inakuwa na chumba cha siri kwa wasichana, iliwe mfano hata kwa mikoa mingine na taifa kwa ujumla.

Pia aliwaasa wazazi, walezi na waalimu kueneza elimu hiyo ili watoto waelewe vizuri umuhimu wa usafi wakati wa hedhi, jambo ambalo litawafanya wawe na furaha, afya na usafi, hivyo kuondokana na mazoea ya kujinynyapaa na kulifanya la siri.

"Tuondokane na baadhi ya mila zetu potofu zinazolifanya suala la hedhi kuwa la siri, inatakiwa kuanzia sasa watoto wa kike wabebe begi lenye vifaa mbalimbali vitakavyowasaidia wakati wa hedhi, ikiwemo khanga, pedi, vitambaa na mtandio.
"alisema Safari.


"Inabidi sote tuwe mabalozi kwa kuongea na watoto, tutunze afya na usafi wao, kwani hao ndiyo viongozi wa taifa letu la kesho
. Bila kuwa na afya njema hatutakuwa na viongozi imara wa  Taifa letu."Alisisitiza Safari.

Dhima na lengo la TGGA ambayo ina wanachama zaidi 100,000 nchininni kuwajengea wasichana nafasi ya kujithamini, ari ya maendeleo, uzalendo kwa nchi na kujiamini.


 Wanafunzi wakiimba wimbo wa hamasa ya kampeni hiyo
 Mmoja wa wanafunzi akielezea jinsi ya kutumia pedi

 Maandamano ya wanafunzi kwenye Uwanja wa Ilulu
 Wanafunzi wa kike wakiwa na furaha wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo
 Rehema Kijazi wa TGGA Makao Makuu akiwahamasisha wanafunzi wakati wa maandamano
 Wanafunzi wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe wa kuhamasisha matumizi salama ya vihifadhi yaani Pedi


 Viongozi wa TGGA Mkoa wa Lindi wakiwa eneo la uzinduzi wa kampeni hiyo
 Makamu Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa Lindi, Saharifa Mkwango akisherehesha 
hafla hiyo

 Katibu Mkuu wa TGGA Taifa, Grace Shaba akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo kwa kuwaeleza  dhima na lengo la chama hicho kuwaelimisha wasichana kuhusu maadili mema na matumizi sahihi ya pedi wakati wa hedhi.
 Baadhi ya wazazi miongoni mwao wakiwemo walimu wakisikiliza kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na mgeni rasmi

 Girl Guids kutoka Rwanda, Uganda na Madagascar wakihamasisha matumizi ya pedi wakati wa hedhi

 Mgeni rasmi, Thomas Safari akihutubia
 Safari akizindua rasmi kampeni hiyo kwa kufungua kasha lenye pedi
 Mgeni rasmi akikabidhi makasha yenye pedi yaani vihifadhi kwa wanafunzi wa shule mbalimbali Wanafunzi wakisakata muziki wakati wa kampeni hiyo

 Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi waliokabidhiwa makasha ya pedi zitakazogawiwa shuleni kwao

 Girl Guids wakiwa katika picha ya pamoja

 Katibu Mkuu wa TGGA Taifa, Grace Shaba akisaidiana na mwanafunzi Caren Seki kumwagilia mti alioupanda katika shule ya Msingi Mtuleni
Mgeni rasmi, Thomas Safari akipanda mti wa kumbukumbu katika Shule ya Msingi Mtuleni
Girl Guids kutoka Rwanda, Madagascar na Uganda ambao wapo nchini kwa mpango wa kubadilishana uzoefu wakipanda mti wa kumbukumbu katika shule ya msingi Mtuleni, Lindi

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO