WAFANYABIASHARA  wa Kigoma na Burundi wameunda kuunda kamati maalum ya kushughulikia changamoto na kero mbalimbali zinawakabili kwenye mpaka wa nchi hizo.
Kamati hiyo imeundwa baada ya mijadala mikali kuhusiana na masuala ya biashara baina yao.
Uamuzi wa kuwa na kamati hiyo umetokana na kuwapo kwa malalamiko mbalimbali ambayo yanatakiwa kuratibiwa na kupatiwa majibu. Miongoni mwa malalamiko hayo ni kuzidi kwa rushwa. 
Akieleza matatizo na kero zinazowakabili wafanyabiashara wa mkoa Kigoma kuvuka mpaka kwenda kufanya biashara nchini Burundi Mratibu miradi wa shirika lisilo la kiserikali la Nyakitonto Youth,Ramadhani Joel alisema kuwa nchi zote mbili zinazo fursa kubwa kwa wafanyabiashara wake lakini kero wanazokumbana nazo mpakani ni kikwazo kikubwa katika maendeleo ya biashara.
Kwa upande wake Mkuu wa msafara wa wafanyabiashara hao kutoka nchini Burundi,Jacqueline Ndaizeye alisema kuwa kumekuwa na shida ya wafanyabiashara kutoka Burundi kukamatwa kwa madai ya kutokuwa na vibali mbalimbali wakati kuna utaratibu wa ujirani mwema kwa wafanyabiashara wa mipakani kuvuka kutoka Burundi kuingia nchini.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO