WANAWAKE wawili wameuawa kw akucharangwa na mapanga na mmoja wameondoka na kiganja cha mkono wake wa kulia.

Mauaji hayo yamefanyika katika kata mbili tofauti wilayani Igunga mkoani Tabora.

Mtendaji wa kata ya Tambalale Salumu Kitindi alimtaja mama aliyeuawa kuwa ni Elizabeth Charles (45) mkulima wa kijiji cha Tambalale katika kata hiyo ya Tambalale tarafa ya Nsimbo.

Alisema watu wasiojulikana walivamia nyumbani kwa mama huyo na kumshambulia kwa mapanga hadi kufa na kukata kiganja cha mkono wa kulia na kuondoka nacho.

Tukio la pili limetokea Busomeke.

Mtendaji wa kata ya Mwisi, Issa Omary alisema katika kata yake mama mmoja Suzana Alex (24) mkulima mkazi wa kijiji cha Busomeke tarafa ya Simbo ameuawa kwa mapanga kwa kukatwa sehemu mbalimbali za mwili wake huku mume wake John Matheo (27) akijeruhiwa vibaya kulazwa hospitali ya Mission ya Ndala iliyoko Nzega.


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO