Meneja Masoko ya Airtel, Anethy Muga (kulia) na Meneja wa chapa wa Airtel, Arnold Madale (kushoto) wakionyesha vocha mpya ya Airtel Tabasamu itakayouzwa kwa bei ya shilingi mia mbili tu. Katikati  ni Meneja  Uhusiano wa Airtel , Jackson Mmbando

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel jana wamezindua vocha ya kiwango cha chini kabisa kwa wateja wa simu za mkononi  hapa nchini ijulikanayo kama tabasamu yenye thamani y ash 200 tu.
Vocha hiyo mpya ya muda wa maongezi  ni kwa ajili ya wateja wake wa malipo ya awali nchini.

Vocha  hiyo mpya ya TABASAMU inayopatikana kwa shilingi 200 kwa sasa ipo kwa wachuuzi wote wa vocha za Airtel .

Akizungumza wakati wa uzinduzi, Meneja Masoko wa Airtel , Aneth Muga alisema kampuni hiyo inajisikia fahari kuzindua na kuitambulisha sokoni vocha ya muda wa maongezi ya shilingi 200.

Alisema ana imani kuwa vocha hiyo  itawapatia wateja Tabasamu na uhuru wa kuwasiliana na ndugu jamaa marafiki au wale wajasiriamali kuweza kuitumia kupanga mipango yao wakati wowote mahali popote kwa gharama nafuu.


“Tunatambua mawasiliano ya simu ni muhimu katika kuendesha shughuli zetu za kila siku na hivyo  kuboreshwa  kwa viwango vya vocha kutasaidia  sana kuchochea upatikanaji wa huduma ya mawasiliano kwa wote. Tunataka kuendelea kutoa huduma bora za kibunifu na zenye kukidhi mahitaji ya wateja wetu huku tukiwawezesha kutatua changamoto zao za kila siku”. Alieleza  Muga

Kuingizwa kwa vocha za shilingi 200 sokoni kutawawezesha zaidi ya watanzania milioni 10 kuunganishwa na huduma za mawasiliano na kufurahia ofa mbalimbal zinazotolewa na Airtel.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO