NCHINI Tunisia, wanawake vijana na wale wanaosubiri kuolewa wanatarajiwa wanapoingia katika ndoa kuwa bado na bikira zao.
Kutokana na shida hiyo kumezuka biashara kubwa ya kutengeneza bikira upya kwa kufanya operesheni ndogo.
Yasmine (Sio jina lake la ukweli) anaonekana kuwa na shaka kubwa katika uso wake ni kama anaweweseka vile.Amekuwa akiuma vidole vyake na kila mara kuangalia simu yake ya mkononi.
"Nafikiria hiki ninachoenda kukifanya  ni uongo na ninakua na shaka sana," anasema.
Tuko katika ghrofa ya nne ya kliniki binafsi mjini Tunis, kiliniki inayotoa huduma  ya magaina (gynaecology).Hatukuwa sisi opeke yetu walikuwapo wanawake wengine wanasubiri katika chumba hicho kilichohanikizwa na rangi ya poda,Wote wanasubiri kuwaona wataalamu.
Yasmine ananiambia kwamba anafanyiwa operesheni ya kurejesha bikra yake (hymenoplasty). 
Kwa mujibu wa Yasmine amebakiza miezi miwili kufikia tarehe ya ndoa yake na anahofu kwamba  mume wake atajua kwamba yeye si bikira na ataachika. 
Binti huyu wa miaka 28 amefika katika kliniki hii kurejesha bikira yake huku bado akiwa na shaka kwamba mume wake anaweza kuja kugundua katika siku za baadae.
"Siku moja bila kujitambua nitamweleza ukweli mume wangu katika mazungumzo," anasema. "Au mume wangu anaweza kuwa na shaka."
Shinikizo
Kumekuwepo na taarifa kwamba baadhi ya wanawake wanaachika mara tu baada ya kuolewa kwa sababu waume zao wanawatilia shaka kwamba hawakuwa na Bikra.
 Pamoja na ukweli kuwa tunaishi katika dunia ya kisasa zaidi lakini jamii iliyopo katika masuala ya ufanyaji mapenzi kwa wanawake hatuishi katika dunia hiyo anasema msosholojia Samia Elloumi.
Yasmine alikuwa amezaliwa katika familia ya kisasa zaidi na  kuishi ughaibuni kwa kipindi kirefu cha maisha yake ya utoto na ujana. Anahofu kwamba mchumba wake atamtema kama atajua kwamba milango iko wazi na kwamba alishawahi kuwa na uhusiano na wanaume wengine.
"Nimekutana na mtu mmoja na nimekaa naye," anasema. "Wakati ule nafanya mambo hayo wala sikufikiria shinikizo kubwa la kiutamaduni lililipo katika jamii yangu na nini matokeo yake, yaani kutatokea nini.
"Sasa ninaogopa kwelikweli. Kama nitamwambia kwamba siko bikira nimeshaona wengine nina hakia ndoa yangu itafutwa."
Yasmine  atalazimika kulipa  dola 400 (£310) kwa ajili ya operesheni hiyo ambayo itachukua dakika 30. Amekuwa aki akiweka akiba ya fedha kwa miezi kadhaa sasa bila kumweleza mchumba wake wala familia yake ili kufanikisha shughuli hiyo.
Daktari atakayefanya shughuli ya kurejesha bikra ya Yasmine ni daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake (gaina)  Rachid (tunamuita hivyo katika haya maandishi) atamfanyia na kwa kawaida daktari huyu hufanya shughuli hizi mara mbili kwa wiki.
Rachid anasema kwamba asilimia 99 ya watu wanaokuja kufanyiwa kazi hiyo wanafanya kutokana na hofu ya kutia aibu familia na ndugu zao.
Wapo wengi ambao kama Yasmine wanatafuta muafaka wa kuonekana kuwa mabikira wakati sio.
Lakini pamoja na kuujua uanamke mapema, bikira huweza kutatuka wka sababu nyingine nah ii husababisha maneno mengi kutoka kwa wasioelewa, wakituhumu wanawake kwa kutokuwa waaminifu katika maisha yao kabla ya kukutana na mwanaume katika ndoa.
"magaina wanaweza kabisa kuripea bikira. Hakuna cha ajabu hapa," anasema Rachid. "Lakini wapo baadhi ya madaktari hawakubaliani na operesheni hizi lakini mimi nafanya kwa kuamini kwamba suala la ubikira si suala la utakatifu kihivyo.
"Mimi inaniudhi sana. Haya ni matunda ya mfumo dume uliojificha katika masuala ya dini . Ninasema hilo kwa uhakika na nitaendelea kupambana na mfumo huo." Akimaananisha kuendelea kuwapa ‘bikira’ feki wanaokuja kutafuta.
'Unafiki'
Tunisia  inaheshimika kwamba ndio kinara za haki za wanawake kwa upande wa Afrika kaskazini, lakini ukumbatiaji wake wa dini na utamaduni kumefanya wanawake kuendelea kubaki bikra mpaka watakapoolewa.
Aidha kuna kifungu katika katiba ya Tunisia ya kuridhia talaka kama mtu atabaini kwamba mke wake hakuwa na bikra.
Mwanasosholojia Samia Elloumi anasema: "katika jamii hii ya Tunisia, ambayo ni jamii iliyopo wazi, sasa tunaingia katika unafiki.
"Kuna kiwango kikubwa cha uzingativu wa masuala ya zamani ambayo hayawezi kujieleza kisawasawa wakati watu wanadai wanaishi katika dunia ya kisasa.Lakini hata hivyo hakuna usasa katika suala la wanawake kubaki bikra na uhuru wake."
Katika chuo kikuu cha umma nilikutana na Hichem. Kijana huyu wa miaka 29 nilimuuliza kama anajali atakapomkuta mchumba wake si bikra.
"Kwangu mimi najali , ni muhimu sana," anasema.
"Kama nitagundua kwamba yeye si bikira baada ya ndoa sitamwamini tena. Nitaona  huo ni usaliti. Siamini katika operesheni za kuriopea bikra.Sidhanui kama inasaidia."
Mwanafunzi mwingine karibu naye , Radhouam,anasema tamaduni za kiasili za Tunisia zinamkandamiza sana mwanamke.
"kwangu mimi huu ni unafiki," anasema. "Vijana wa kiume wanaweza tu kutembea na mtu yoyote kabla ya ndoa sasa kwanini tuwalaumu vijana wa kike kwa kukosa bikra? Kwani wao hawana haki ya kuzurura?"

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO