Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma Vumilia Nyamoga (kulia) akimkabidhi mwenge wa uhuru Mkuu wa Wilaya ya Chemba Simon Odunga wakati wa mwenge wa uhuru ulipofika wilayani humo .
WILAYA ya Chemba ambayo ilikuwa inapata huduma za mafuta kutoka Kondoa sasa itaanza kupata huduma hiyo wilayani hapo baada ya kukamilika kwa ujenzi  wa kituo cha mafuta kinachomilikiwa na Mtanzania  Yunus Mpala.

Wilaya hiyo tangu ilipoanzishwa mwaka 2012 imekuwa ikipata huduma hiyo wilaya ya Kondoa iliyopo takriban kilometa 43.

Mradi huo ulianza Aprili 2017 mpaka utakapokamilika utagharimu Sh milioni 500.
Akitoa taarifa katika mbio za mwenge hivi karibuni Mkuu wa wilaya ya Chemba, Simon Odunga alisema wilaya hiyo yenye wakazi 250,000 tangu ilipoanzishwa mwaka 2012 ina miundombinu michache na mingi bado inahitaji kujengwa.

Alisema kwa wakati nchi inapoingia kwenye uchumi wa viwanda ni vyema wawekezaji wazalendo wakajitokeza kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ili kusogeza huduma karibu na wananchi.

Akizungumza baada ya kuzindua na kukagua ujenzi wa kitui hicho, Amour alisema katika mradi wa ujenzi unaoendelea ni vyema mmiliki wa kituo hicho akazingatia afya za wananchi.
“Nimekagua jengo lakini wafanyakazi hawana mavazi yoyote ya kujikinga na ajali au hewa chafu, afya za wafanyakazi lazima zipewe kipaumbele” alisema

Pia alitaka kituo hicho kuwa na vitu vyote vinavyohitajika kuwa kwenye vituo vya mafuta kama vifaa vya kuzimia moto na kupata vibali vyote kabla ya kuanza kwa biashara.
 “Tunataka hiki kiwe kituo cha mfano, kiwe kinajaza mafuta kwenye magari ambayo hayana abiria ndani” alisema
Source:Sifa Lubasi, ChembaPost a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO