HUYU ni mdada ambaye  amekuwa akionekana katika filamu nyingi zilizoenda shule za Nollywood. Pamoja na kuwa maarufu katika sinema amepata mafanikio makubwa katika shughuli zake huku akiwa na mamilioni ya mashabiki katika twita, instagramu na hata fesibuku.

Genevieve Nnaji amezaliwa Mei 3, 1979 katika familia ya Theophilius na Bebedatte Nnaji huko Mbaise, jimbo la Imo , Nigeria. Baada ya uzazi wake wazazi wake hawakukaa sana katika eneo hilo na familia ikahamia mjini Lagos.

Nnaji ametoka katika familia yenye watu saba na yeye ni mtoto wa katikati. Familia yake ilikuwa watu wa kipato cha kati mama akiwa ni mwalimu wa shule za awali na baba yake mhandisi.

Mdada huyu ambaye ana mtoto mwenye umri wa miaka 22  amepitia shule ya Methodist Girls College huko Yaba, Lagos. Kisha aliendelea hadi chuo klikuu cha Lagos ambako alipata Bachelor of Arts degree katika Creative Arts.

Wakati anasoma inaelezwa kuwa alitafuta nafasi nyingi za kuigiza kwa kuhudhuria kila wito au miito aliyokuwa anaiona ina maana kwake ya uigizaji lakini hakufanikiwa, ingawa maelezo yanasema kwamba alianza uigizaji katika miaka ya 1980 kwa kuanzia katika shoo ya televisheni ya  ‘Ripples’ .

Shoo hii ilikuwa ni kiboko na kiukweli alianza akiwa na miaka minane. Kazi hasa ya uigizaji wenya maana na tija alianza mwaka 1998 alipoigiza katika sinema ya Most Wanted.

Baada ya kufanya vyema katika sinema hii alipata kazi mfululizo na mpaka tunaandika habarik hii mdada huyu ameigiza katika sinema zaidi ya 80. Miongoni mwa sinema zake zilizofanya vyema ni Mark of the Beast, Last Party, Sharon Stone na Ijele.

Kutokana na kazi zake hizo Genevieve ametajwa na kupokea tuzo kadhaa ikiwamo ya muigizaji bora wa kike inayotolewa na  City People  mwaka 2001, na muigizaji bora wa kike katika nafasi ya uongozi, tuzo inayotolewa na Africa Movie Academy Awards  ya mwaka 2005.


Mwaka 2009, Genevieve Nnaji  alihojiwa ndani ya kipindi cha The Oprah Winfrey Show, akiwa ni Mnaijeria muigizaji wa kike wa kwanza kuzungumza katika shoo hiyo inayotazamwa na mamilioni ya watu.

Kwa mtu ambaye amepata mafanikio makubwa katika uigizaji, angeliweza kubaki huko lakini yeye akaenda mbali zaidi kw akuwa mzalishaji na mtengenezaji wa sinema yaani projuza na dairekta.

Mwaka 2015 alikuwa ni mmoja wa maprojuza na muigizaji kinara katika sinema ya Road to Yesterday, sinema ambayo ilipata tuzo ya sinema bora ya Afrika Magharibi katika kinyang'anyiro cha sinema bora katika tuzo za mwaka jana za Africa Magic Viewers Choice .

Mwaka huu 2017 mdada huyu amepanga kuongoza sinema nyingine ya Lion Heart.


akiwana Ramsey

Genevieve pia ametokea katika matangazo kadha ya biashara yenye fuba nene kama Pronto and Omo. Pia alikuwa ni kisura wa Lux kwa mwaka 2004(Face of Lux  2004 ) na Face of MUD kwa mwaka 2010.

katika mafanikio yake kuanzia mwaka 2008,amekuwa akiendesha lebo yake ya mavazi ambayo anaiita St. Genevieve. Imeelezwa kuwa laini hii ilianzishwa kumwezesha kutoa kwa wahitaji, sehemu kubwa ya mapato yanapelekwa kwa yatima nchini Nigeria.

Kitu kingine ni kwamba mdada huyu pia ni mwambaji. Mwaka 2004 aliachia albamu yenye kubea jina la utambuzi la One Logologo Line chini ya lebo ya Westside Music Inc.

Ukiangalia mafanikio yake unaweza kujiuliza kweli kuna kitu ambacho hawezi kukifanya maana yake ni kwamba anaonekana kuwa mtu ambaye ana vipaji kibao.

Chimebuka
Pamoja na kuwa na mafanikio makubwa mdada huyu  bado yuko mwepeke na amekuwa akilinda mambo yake binafsi kwa gharama kubwa.Hata habari ya baba wa mtoto wake watu hawaijui kwa uhakika. Mtoto huyu mwenye umri wa miaka 22 anaitwa Theodora Chimebuka Nnaji na mwaka jana aliolewa.


Ukifanya hesabu zako sawa utabaini kwamba Genevieve Nnaji  alimpata binti huyu akiwa na umri wa miaka 16, bado mbichi sana.

katika moja ya mahojiano alisema kwamba hakujua kama ana mimba  kwa kipindi kirefu na hii inatokana na malezi yake ya kikatoliki aliyokuwa nayo.

Pamoja na matata yote, wazazi wake walimkubali mjukuu wao na akawa anaishi na bibi yake ughaibuni. Bibi anatambuliwa kwa jina la Bebedatte.Inaelezwa kuwa Genevieve alitaka kumlinda binti yake na hekaheka za waanfdishi wa habari.

Mpaka kesho hajasema nani ni baba watoto wake na mbaya zaidi ameendelea na tabia za kikatoliki akikataa kabisa kuwa karibu kivile na wanaume.

Na D' banj
pamoja na kuendelea kusubiri  wanahabari bado wanamtesa na tetesi zao wakimuunganisha mara kadhaa na  muigizaji maarufu Ramsey Nouah  na mwimbaji D’banj.


Katika mitandao ya kijamii, mdada ana wafuasi kibao ndani ya Instagram, Facebook na Twitter, na mara kwa mara huweka picha zake na mambo yanayomhusu katika maisha. Instagram: @genevievennaji, ina mashabiki milioni 2.9 . Twitter: @GenevieveNnaji1, ana wafuasi milioni 1.2 na ndani ya Facebook ana watu milioni 2.66 waliopenda kurasa wake. Aidha ana tovuti: www.genevieveofficial.com .

Akiwa na miaka 38 mdada huyu bado ni mrembo wa haja.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO