MWENYEKITI  wa  CCM wa  Mkoa wa  Katavi, Mselemu  Abdalla  na  Meya wa Manispaa ya  Mpanda  Willy  Mbogo waliongoza  mamia ya waombolezaji katika maziko ya mwandishi wa habari  na mtangazaji  nguli wa iliyokuwa Radio Tanzania Dar Es Salaam (RTD) , Lucas Matipa (77) .

Marehemu amefariki dunia jana akiwa nyumbani  kwao wilayani Mpanda katika mkoa wa Katavi na mwili wake kuzikwa  katika makaburi ya Mwangaza yaliyopo  katika  Mji wa Mpanda
katika mkoa wa Katavi ..

 Kwa  mujibu wa wa  kaka wa   marehemu   Padri wa Kanisa Katoliki , Jimbo la Mpanda , Simon Matipa  mauti yalimfika mzee Lucas jana  saa  kumi na mbili na nusu asubuhi nyumbani kwao iliyopo katika Mtaa wa Majengo  katika Manispaa  ya Mpanda  mkoani Katavi .

Padre Matipa alisema  marehemu  mdogo wake alizaliwa   mwaka 1940 mwambao mwa Ziwa  Tanganyika  Tarafa ya  Karema    Wilaya ya  Mpanda ambayo sasa ni   Wilaya ya    Tanganyika .

 “Marehemu alistaafu kazi  ya uandishi na utangazaji  RTD  mwaka  2006 , enzi za uhai wake alifanya kazi na wandishi mbalimbali  miongoni mwa  watangazaji  hao ni  marehemu aliyekuwa Mkurugenzi wa radio hiyo David   Wakati (ambaye  naye ni marehemu ).”

Alisema marehemu mdogo wake  alianza kuugua  tangu mwaka juzi  ambapo alilazimika  kurudi nyumbani (Mpanda) akitokea Jijini Dar es Salaam alikokuwa  akiishi.

Alisema Ibada ya Misa Takatifu ya Wafu  ilifanyika  jana  katika Kanisa   Katoliki  Jimbo la  Mpanda iliyoongozwa na  Paroko  Msaidizi wa  Kanisa hilo  ,Kasisi Dominick Odhiambo  akisadiana  nae (Padre
Matipa ).

Rest in peace Mzee Matipa nakukumbuka 1985 chumba cha Habari Radio Tanzania, Pugu Road Nisalimie wote na pasi shaka utamuona baba yangu Mzee John Luwanda aliyekutangulia. Nyote mlale salama.
Beda Msimbe

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO