Mkuu wa shule Janeth Lubasi akisoma taarifa ya shule na ujenzi
KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa ,Amour Hamad Amour  amempongeza mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mwanzi iliyopo Manyoni mkoani Singida Janeth Lubasi kwa ujenzi imara wa bweni la wasichana katika shule.

Alitoa pongezi hizo wakati alipokuwa akihutubia baada ya kukagua na kuzindua jiwe la msingi la bweni la wasichana baada ya mwenge kuwasili katika shule hiyo.

Kiongozi wa mbio z amwenge Amour akihutubia

"Hongera sana mama...yaani hapa umepata Hosteli. Mimi nimeukubali kwa asilimia mia." alisema Amour.

Awali akitoa taarifa fupi mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge, Mkuu wa Shule hiyo mwalimu Janeth Lubasi  alisema ujenzi wa bweni hilo ulianza tangu mwaka 2010. Uendelezaji wake uliendelea baada ya kuungua kwa bweni la wasichana shuleni hapo mwaka jana.

Kwa mujibu wa kumbukumbu za bologuu moto huo ambao ulianza saa mbili za usiku hadi asubuhi uliteketeza bweni hilo lililokuwa  linakaliwa na wanafunzi wa kidato cha tano na sita  kila kitu cha wanafunzi hao ambao walikuwa madarasani wakijiandaa na mitihani yao ya kawaida ya ndani.

Kiongozi wa mbio za Mwenge amour akiangalia jiwe la msingi baada ya kuzindua

Aidha Mkuu huyo wa Shule alisema mradi huo unajengwa kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali, ikiwemo Halmashauri ya Manyoni, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Wafanyabiashara wa Manyoni pamoja na nguvu za wananchi wa Manyoni.

Alisema mradi  ukikamilika utaweza kubeba jumla ya wanafunzi 50 kwa wakati mmoja ambao ni wanafunzi wa kike wa kidato cha tano na sita wanaokaa hosteli.

Sehemu ya muonekano wa bweni linaloendelea kujengwa

wananchi waliofika kutumbuiza
Shule hiyo ina wanafunzi 672 wa kidato cha kwanza hadi za sita ikiwa ni shule ya mchanganyiko wa wavulana na wasichana, Pia ni kituo kwa walimu waliokazini kwa masomo ya Sayansi, hesabu, Kiingereza na tehama kwa kwa mkoa wa Singida.

Pamoja na kumpongeza mkuu wa shule kwa kazi nzuri ya ujenzi wa bweni pia kiongozi huyo wa Mbio za mwenge kitaifa Amour Hamad Amour ametaka kusimamia vijana kujifunza kwa bidii na kufundishwa uzalendo wa kuijua nchi yao.

“Muwafundishe vijana uzalendo waijue nchi yao” alisema

Mwenge wa Uhuru ulianza mbio zake katika Wilaya ya Manyoni mkoani Singida juzi na moja ya miradi iliyozinduliwa ni kuwekea jiwe la msingi la ujenzi wa Bweni la Wasichana la Shule ya Sekondari Mwanzi.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO