MLIPUKO mkubwa wa kipindupindu ambao haujawahi kutokea una tatizo wananchi wa Yemen kwa sasa.
Shirika la Afya Duniani linasema kwamba huku kila siku kukiibuka wagonjwa wapya wa kipindupindu kufikia watu 5000, wananchi waliokumbwa na ugonjwa huo ni zaidi ya 200,000.
Mpaka sasa watu 1,300 wamefariki dunia robo yao wakiwa ni watoto na idadi inatarajiw akuongezeka zaidi kutokana na huduma duni katika makambi husika.
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yamesema kwamba yanafanya kila linalowezekana ili kuhakikisha kwamba hali inadhibitiwa.
Taarifa ya serikali inasema kiwango cha wagonjwa wakipindupindu haijawahi kutokea.
Katika kipindi cha miezi miwili kipindupindu kimesambaa kila mahali katika nchi hii ambayo tayari imekuwa na hali mbaya kutokana na vita.
Baada ya vita ya miaka miwili ya wenyewe kwa wenyewe, miundombinu imeharibika na  kuliacha taifa hilo katika mazingira magumu sana kiafya.
Hospitali za nchi hii kwa sasa zimejazwa na watoto na wanawake wanaohitaji chakula na kuna kiwangio kikubwa cha lishe duni na kufanya watu na hasa watoto kupatwa na kipindupindu kirahisi.
Ingawa Umoja wa Mataifa umesema utapita nyumba kw an yumba kuwaambuia watu namna ya kukabiliana na kipindupindu kw akuhifadhi mahhji salama ya kunywa, picha ni ngumu kutokana kukosekana kwa maji salama.
Wenghi wa watu wanaopata ugonjwa huu mapema zaidi kama sipogundulika na kuanza matibabu mara moja.
 Vita hii imesababisha watu kati ya milioni 18 na 20 kupoteza makazi na kutafuta msaada.
Kwa sasa watu milioni 7 wapo katika hatari ya kupatwa na balaa njaa kutokan ana ukame na kukosa muda w akujisughulisha na mashamab kutokana na vita inayoendelea.


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO