MBUNGE wa jimbo la Mtama Nape Nnauye na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Jordan
Lugimbana wameongoza mamia ya waombolezaji kwa ajili ya kuuaga mwili
wa marehemu wa shabiki maarufu na timu ya soka ya Yanga na kada wa CCM
marehemu Ally Mohamed  maarufu Ally Yanga.
Waombolezaji hao walijitokeza katika hospitali ya mkoa wa
Dodoma,pamoja na mashabiki wa timu hiyo,wakwemo viongozi wa chama cha
mapinduzi mkoa wa Dodoma.
Akizungumza wakati wa kuaga mwili wa Alyy Yanga aliyepata ajali juzi
eneo la Chipogolo lililopo Wilayani Mpwapwa mkoani hapa,Sheikh Mkuu wa
mkoa wa Dodoma Mustapha Rajabu alitoa pole kwa wanayanga wote pamoja
na CCM kwa ujumla huku akisema hatuna sababu ya kusikitika
tunachotakiwa ni kumuombea kwa sababu amemaliza kazi yake duniani.
Alisema Ally Yanga alikuwa ni kipenzi cha watu,hususani familia yake
na familia ya mpira pamoja na makada wa chama cha Mapinduzi,najua
tumeumia sana, lakini hiyo yote ni kazi ya Mungu ambayo haina makosa.
"Sisi sote tuwapitaji hapa duniani, mwenzetu ametangulia nasisi
tutafuata, kinachotakiwa ni kumuombea,"alisema Sheikh Rajabu.
Naye Mwenyekiti wa Yanga moa wa Dodoma Fred Mushi alisema ni pigo
kubwa kwa wanachama wa Yanga, kwa sababu Ally Yanga alikuwa ni shabiki
mzuri,na alikuwa akihesabika kama mchezaji wa 12 kwa sababu ya hamasa
zake za ushangiliaji pale anapokuwa uwanjani.
"Yanga imepoteza mtu muhimu sana katiaka mchezo wa soka, lakini hakuna
jinsi imetokea tunapaswa kumuombea,"alisema Mushi.
Kwa upande wa Katibu wa chama cha soka mkoa wa Dodoma DOREFA Hamis
Kissoy alisema familia ya michezo imepoteza mtu muhimu sana, ambaye
alipenda kujitoa katika suala zima la michezo kwa ujumla.
"Ukioacha Yanga wanamichezo wote tumepata pigo kwa sababu Ally Yanga
alikuwa ni muhamasishaji mkubwa kwenye michezo hususani timu ya taifa
ikiwa na mashindano humkosi uwanjani,"alisema Kissoy.
Hata hivyo aisema kwa niaba ya wanamichezo mkoani Dodoma na Shirikisho
la soka nchini TFF, anatoa pole kwa familia yake, pamoja na klabu ya
Yanga kwa kumpoteza mtu muhimu kwenye michezo.
Ally Yanga alifariki juzi katika ajali ya gari iliotokea eneo la
Chipogolo,mwili wake umesafirishwa jana kuelekea Shinyanga kwa ajili
ya taratibu za mazishi leo.

Mwisho.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO