PROGRAMU YA LIPA KULINGANA NA MATOKEO IMELETA MAGEUZI KATIKA SEKTA YA ELIMU

SEKTA ya Elimu ni miongoni mwa vipaumbele muhimu vya maendeleo vilivyopewa mkazo na Serikali ya Awamu ya Tano katika kufanikisha utoaji wa ...

SEKTA ya Elimu ni miongoni mwa vipaumbele muhimu vya maendeleo vilivyopewa mkazo na Serikali ya Awamu ya Tano katika kufanikisha utoaji wa huduma muhimu kwa wananchi ili kuchochea adhma ya kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Kupitia Sera Mpya ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, Serikali imeazimia kutekeleza mipango mbalimbali ikiwemo utoaji elimu ya msingi bila ada, kuongeza ubora wa elimu kwa kuimarisha ukaguzi shuleni, na kuboresha miundombinu.
Aidha Serikali ilikusudia pia kuhakikisha upatikanaji wa vifaa stahili vya kufundishia na kujifunzia, kuongeza ubora wa walimu kwa kutoa mafunzo, motisha  pamoja na udhibiti wa taaluma ya ualimu.
Ili kufanikisha malengo hayo, Serikali imekuwa ikitekeleza miradi, mipango na programu mbalimbali za elimu ili  kuleta maendeleo ya haraka ya rasilimali watu kwa kutayarisha idadi ya kutosha ya Watanzania walioelimika na kupenda kujielimisha.
Miongoni mwa Programu hizo ni Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo inayotekelezwa na Serikali katika kipindi cha miaka mitano 2014-18 iliyokusudia kuimarisha usimamizi wa raslimali fedha na manunuzi ya umma katika mipango ya elimu kwa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa.
Programu hiyo inatekelezwa katika sekta za elimu ya msingi na Sekondari na kufadhiliwa na Benki ya Dunia, Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Sweden (SIDA) na Ubalozi wa Uingereza 
Aidha programu hiyo pia imelenga kuanzisha njia ya moja kwa moja ya ugharimiaji elimu inayolenga kuipa motisha Serikali katika utekelezaji wa mipango inayolenga matokeo ya haraka.
Maeneo muhimu yaliyochaguliwa kupitia programu hiyo ni pamoja na utoaji wa zawadi na motisha ya fedha na zisizo za fedha kwa walimu na shule zilizofanya vizuri, kutoa mafunzo kazini kwa walimu na kuimarisha mfumo wa Serikali na kufanya ufuatiliaji ya utolewaji na utumiaji wa fedha za ruzuku.
Aidha kupitia programu hiyo Serikali imekusudia kuimarisha uwazi wa matokeo ya mitihani kwa shule za Msingi na Sekondari na kufanya tathimni ya kujua kusoma, kuhesabu na kuandika kwa shule za halmashauri zilizoteuliwa katika zoezi hilo.
Katika kuhakikisha kuwa Programu hiyo inaleta tija iliyokusudiwa, Serikali imeanisha vipaumbele vikuu vitatu vinavyotumika katika kila Halmashauri ili kupima matokeo na kutoa motisha (fedha) kulingana na mahitaji na matumizi iliyojiwekea.
Vipaumbele hivyo ni pamoja na upangaji wa walimu katika shule zenye mahitaji, upelekaji wa ruzuku ya fedha za shule kutoka hazina pamoja na uwezo wa halmashauri kukusanya takwimu kwa usahihi na kuziweka mtandaoni kwa wakati.
Taarifa ya Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inasema kuwa hadi sasa kiasi cha Tsh. Bilioni 90 zimeweza kupatikana kutokana na Serikali kutekeleza vipaumbele vyake kwa ufanisi kulingana na fedha za motisha zinazotolewa katika kila Halmashauri iliyopo katika mradi huo.
Aidha Serikali imetoa kiasi cha Tsh. Bilioni 22  za motisha kwa Halmashauri 179 zilizohakikiwa kwa mwaka 2015/16 ambapo zilitolewa kufuatana na viwango vya utekelezaji wa viashiria vya utendaji katika sekta ya elimu.
Akiwasilisha Hotuba ya makadirio ya Bajeti ya mwaka 2017/18, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI George Simbachawene anasema Programu ya Lipa kulingana na matokeo imekusudia kuongeza ufanisi na uwajibikaji wa kutoa elimu nchini na kujenga uwezo wa Serikali wa kutekeleza vipaumbele vyake ilivyojiwekea.
Anasema Programu hiyo imeweza kuongeza kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Darasa la Nne na Darasa la Saba, kutokana na jitihada zilizofanywa na Serikali katika kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.
“Ufaulu katika Mtihani wa Taifa wa Kumaliza Shule ya Msingi umeongezeka kutoka asilimia 68.4 mwaka 2015 hadi  asilimia 70.36 mwaka 2016. Wanafunzi wote waliofaulu Mtihani huo wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka 2017” anasema Simbachawene.
Aidha Simbachawene anasema kupitia Programu hiyo, Serikali katika mwaka 2016/17 imeweza  kutoa mafunzo kwa  Maafisa Elimu Vifaa na Takwimu 370 kutoka Halmashauri 184 na Maafisa Elimu  Taaluma Mikoa 26 kuhusu matumizi ya mfumo wa uingizaji na utoaji wa takwimu kwa njia ya kielektroniki ili kuboresha upatikanaji wa takwimu za Elimu kwa usahihi na kwa wakati.
Kwa mujibu wa Simbachawene anasema Ofisi yake pia imeweza kusambaza nakala za vitabu 1,412,832 vya masomo ya Historia, Jiografia na Kiingereza kwa Kidato cha Kwanza hadi cha Nne na vitabu 159,737 vikiwemo 83,189 vya masomo ya sayansi na vitabu 76,548 vya masomo ya sanaa kwa Kidato cha Tano na Sita zilizopo katika Halmashauri 184 nchini.
Kuhusu ujenzi wa Maabara, Simbachawene anasema Serikali kupitia Mpango wa Uimarishaji wa Stadi za Kusoma Kuandika na Kuhesabu imefanikiwa kununua vifaa vya maabara vyenye thamani ya Tsh. bilioni 16 na kuvisambaza katika shule 1,696 zilizokamilisha ujenzi sawa na asilimia 47 ya shule za sekondari 3,602.
“Shule za Sekondari nchini zinahitaji maabara 10,840 na zilizopo kwa sasa ni 5,562 sawa na asilimia 51.3 na upungufu ni maabara 5,278 ambazo zinaendelea kujengwa” anasema Simbachawene.
Simbachawene anasema kupitia kupitia Mpango wa Elimu wa Lipa kwa Matokeo, Serikali kwa kushirikiana na SIDA, Ubalozi wa Uingereza na Benki ya Dunia imeweza kutumia kiasi cha Tsh. Bilioni 21 kwa ajili ya upanuzi wa miundombinu  katika Shule 85 za Sekondari za Kidato cha Tano na Sita nchini.
Akifafanua zaidi Simbachawene anasema katika mwaka wa fedha 2016/17, Serikali imetuma kiasi cha Tsh. Bilioni 36.8 katika akaunti za Shule za Sekondari Kongwe 23 kwa ajili ya ukarabati na Tsh. Bilioni 3.5 zimepelekwa katika Shule saba (7) za Sekondari za Ufundi kwa ajili ya ukarabati wa karakana.
Dhana ya Programu ya Lipa kulingana na Matokeo ikieleweka kwa wadau wote na kufanyiwa kazi kulingana na viashiria vilivyowekwa itasaidia kuijengea Serikali utamaduni wa kufanya kazi kwa matokeo na kutekeleza malengo iliyojiwekea kwa wakati.
Aidha Programu hiyo itaisaidia Serikali kufikia azima na kusudio la kuboresha kiwango cha elimu itakayoleta ushindani na mchango mkubwa katika maendeleo ya viwanda nchini. 
Source:Ismail Ngayonga
MAELEZO
DAR ES SALAAM
27.6.2017



COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,301,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4810,habari. dodoma,23,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: PROGRAMU YA LIPA KULINGANA NA MATOKEO IMELETA MAGEUZI KATIKA SEKTA YA ELIMU
PROGRAMU YA LIPA KULINGANA NA MATOKEO IMELETA MAGEUZI KATIKA SEKTA YA ELIMU
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2017/06/programu-ya-lipa-kulingana-na-matokeo.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2017/06/programu-ya-lipa-kulingana-na-matokeo.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy