WAKATI tamasha la mwaka huu linaanza na sinema ya Kitanzania T Junction, sinema iliyoongozwa na  Amil Shivji, ambaye pia ni mwalimu wa masuala ya sinema, jicho la watanzania limebaki kujiuliza kama sinema hii inaweza kuitoa kimasomaso Watanzania.

Kwa takribani miaka zaidi ya  15 sinema zilizokuwa zinanyakua tuzo zimekuwa za nje huku zilizotengenezwa na watanzania katika mazingira ya Tanzania zikiambulia patupu au pengine kutoonwa.

Ndani ya sinema hii Baada ya kifo cha baba ,Fatima anakutana na rafiki asiyemtarajia hospitaini kwa jina Maria. Kutokana na kumshiba, anajikuta akirudi hospitali kila mara kula gumzo na mdada huyu ambaye anampeleka katika visa vye hisia kubwa.

Ndani kuna mapenzi ndani kuna ghadhabu ndio simulizi hili kwenye maisha ya jamii za kawaida kabisa katika maish aya watanzania.

Kijiweni wanajulikana kwa kazi zao nzuri na nyingi zimeshaingia katika nafasi nzuri ya ushiriki wa kimataifa. Kuna samaki mchangani na Aisha.

Kijiweni kwa namna wanavyokwenda wanapanda kila wanapotoa projekti na h ii ndio  maulizo ya msingi je baada ya miaka yote hii itaweza kututoa watanzania manake mpaka inafikia mahali inafanyiwa primia na tena ndio kifungua pazia si mchezo.

Katika maisha ya karibuni, kutokana na ushiriki hafifu wa watengeneza sinema wa Kitanzania, tamasha lililazimika kutoa nafasi kwa Swahili Movies kwa kuanzisha Tuzo za Bongo.

Hata hivyo pamoja na kuanzishwa kwa tuzop hizo bado ushiriki umeendelea kuwa hafifu ama kwa kutoleewa fursa zinazopatikana kwa kuingia katika jukwaa la ZIFF au woga wa kukumbana na ukweli kuhusu ubora wa sinema zetu.


T junction kwa mujibu wa mtendaji wa ZIFF, Daniel Nyalusi ni miongoni mwa sinema za Kitanzania zenye mahadhi ya Afrika ambazo zimeingia katika katika mashindano.

“ Tuna sinema kama ishirini hivi lakini ni tano tu zina mahadhi hasa ya kuwa katika mashindano, zinaweza kushindana kimataifa” alisema Daniel Nyalusi wakati wa mahojiano na waandishi wa habari juzi kwenye uzinduzi wa tamasha  la kimataifa la filamu  al maarufu kama tamasha la majahazi (ZIFF) lililofanyika  Goethe-Institut jijini Dar es salaam jana

Alisema kuna kazi kubwa ya kwuezesha Watanzania kuchukua nafasi zao katika soko la kimataifa, lakini pamoja na kazi hiyo wahusika hawachukulii maanani kutokana na kutotumia fursa zilizopo.

Alisema katika mazungumzo hayo kwamba pamoja na  tuzo katika madaraja mbalimbali safari hii kuna dola elfu 14 ambazo zinatawanywa katika tuzo mbalimbali lengo likikwa kuingizaa ushawishi na kupunguza makali ya utengenezaji wa sinema.

Alisema kama watanzania wnagelitumia nafasi za kila mwaka na kujumuika na watu wengine ambao tayari wapo mbele ingelikuwa ni salama zaidi kwa tasnia na tungelijua wapi pa kuuza na aina ya baihdaa zinaoztakiwa.

Alisema fursa zilizopo katika tasnia ni pamoja na elimu ya utengenezaji sinema, elimu ambayo kila mwaka inatolewa kwa kundi al watu ambaow ameomba kufanyiwa hivyo.

Mwaka huu makongamano mbalimbali ya utengenezaji wa filamu pamoja na kuwapo kwa Maisha Film Lab. Pia kutakuwapo na  kongamano la uzalishaji wa dokumentari, utengenezaji wa video ya dakika moja, vijana kukutana na wazee, shule za utengenezaji sinema, kongamano la uigizaji,muziki katika sinema kongamano la wanawake watengeneza sinema na masuala ya masoko utafutaji wazo la sinema na usambazaji.

Pamoja na sinema, utofauti mkubwa upo katika tamasha hili ambalo pia limefanya Patna na  tamasha la Busara , matamasha mawili yenye malengo ya sanaa yanayofanyikia Zanzibnar.

Ndani ya Tamasha la majahazi kuna makongamano mbalimbali yanayohusu utamaduni na hasa mijadala wazi ya wanawake, watoto na pia utulivu na busara za kisiasa.

Kimsingi ni tamasha ambalo, limesheheni mambo mbalimbali ambayo naamini pia kwamba yanaweza kuwa vyanzo vya utengenezaji wa sinema. Mfano mwaka huu kuna historia ya urithi na amani Zanzibar na mazungumzo bayana ya changamoto za siasa za kichochezi.

Maonesho mbalimbali ya picgha yenye habari za ndani zaidi kuliko maelezo ni sehemu ya kuangalia mnyumbuko wa utamaduni na hata hizi picha zinazoweza kichocheo cha wazo la sinema za kesho.

Pamoja na mambo yanayosababisha jahazi lisonge mbele zaidi katika utamaduni na sinema tuzo zinazotolewa ndizo zinazoipa heshima kubwa tamasha hili.

Kuna tuzo mbalimbali:

TUZO ZA ZIFF (JAHAZI LA DHAHABU NA FEDHA)
Best Feature film itatolewa kwa hisani ya Showmax
Best Short film
Best Documentary
Best Feature from Dhow Countries
Best Short from Dhow Countries
Best Film from International
Best Animation
Best East African Film

TZUO MAALUMU
Hutolewa na majopo ya majaji yanayojitegemea.

Tuzo ya Mwenyekiti au Bibi Kidude Award (Kutoka Bodi ya ZIFF)
Tuzo ya kutukuka (ZIFF Lifetime Achievement Award).  (Kutoka Bodi ya ZIFF )
Tuzo ya Sembene Ousmane :
Taasisi za GIZ na ZIFF zitatoa tuzo kwa filamu tatyu fupi  zilizotengenezwa na mwafrika iwe Afrika au ughaibuni.

Tuzo ya skuli za filamu
Tuzo ya Bongo Movies:
Maarufu miongoni mwa watazama sinema za Kiswahili za Tanzania
Tuzo ya video bomba ya Trace Mziki:
Kwa ajili ya watu wa Afrika mashariki
Tuzo ya Emerson ya Zanzibar:
kwa ajili ya sinema ya jenre yoyote kuhusu Zanzibar iliyotengenezwa Zanzibar au na wazaznzibari wenyewe.
Tuzo za SIGNIS
Ni kwa ajili ya filamu bora ya Kiafrika nay a Afrika Mashariki. Tuzo hizi hutolewa kwa filamu inayoelezea utu na heshima ya binadamu, haki na uvumilivu kupitia sanaa ya sinema

Tuzo za EAFF
hii ni tuzo inayotolewa na jumuiya ya Ulaya kw atamasha la filamu la Kiafrika
Tuzo ya ADIAHA – dokumentari bora iliyotengenezwa na mtengeneza sinema mwanamke wa Kiafrika

Majaji katika tuzo hizo wataoka maeneo mbalimbali duniani ikiwamo Tanzania.

Source:Beda Msimbe

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO