UROHO  wa kuchota mafuta umekatisha maisha ya watu 123 katika mji wa Ahmedpur East nchini Pakistan.
Taarifa kutoka eneo la tukio linasema kwamba baada ya  kugundua kwamba lori lililokuwa likisafirisha mafuta limeanguka, wananchi walikusanyika ili kufyonza mafuta yaliyokuwa yanatiririka.
Wakati wakichota mafuta  moto mkubwa ulilipuka na kulamba wote waliokuwepo katiak eneo hilo.
OPia imeelezwa kuwa mamia ya watu wamelezwa wakiuguza majeraha yam to huo.
Inaaminika watu waliokuwa wakivuta sigara walisababisha mlipukohuo.
Elkopta za jeshi la Pakistan zilikimbizwa katika eneo la tukio ili kusaidia kuwakimbiza hospitalini majeruhi.

Msemaji wa jeshi Meja jenerali Asif Ghafoor  alisema kwamba jeshi liliingilia kusaidia .

Hata hivyo inaaminika kwamba  vifo zaidi vinatarajiw akutangazwa kwa jinsisaid in a tweet.

Magari sita na pikipiki 12 ziliungua vibaya katika eneo hilo.
Imeelezwa baadhi ya watu walioungua wanaweza kutambuliwa kwa kutumia DNA pekee.
Polisi wanasema kwamba lori hilo lilikuwa limebeba lita 25,000 za mafuta likisafirishwa kutoka Karachi hadi Lahore.
Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Kachi Pul  kiasi cha kilomita nane kutoka Ahmedpur East, huko  Punjab katika wilaya ya Bahawalpur.
Imeelezwa kuwa watu waliokuwapo hapo walichukua mitungi kwenda kujaza mafuta na kuwapigia vijiji jirani ambao walifika kwa wingi.
Imeelezwa kuwa juhudi za polisi kuwatenganisha watu na lori hilo kwa kuwazuia kulikaribia zilishindwa na wananchi wakalizunguka wakitwaa mafuta.

&&&&&&&&&&&&&

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO