WASHINGTON, Marekani
Sasa ni dhahiri kwamba mpango wa  afya wa Rais Donald Trump wenye lengo la kuondoa mpango aliouanzisha Barack Obama utashindwa baada ya kubainika kwamba watu maskini wasiokuwa na bima ya afya kutokana na mpango mpya wa Trump watafikia milioni 22 ifikapo mwaka 2026.
Kutokana na kubainika huko baadhi ay waseneta wa chama cha republican wamesema dhahiri kwamba hawataunga mkono mapendekezo mapya ya bima ya afya kwa wananchi wa Marekani.
Maseneta wawili wa Republican, Senata Susan Collins wa Maine na Rand Paul wa Kentucky,wamesema jana kwamba wataupinga muswada huo mpya wakiungana na Senata Dean Heller wa Nevada ambaye amesema kwamba ataupinga mpango kutokana na athari zake kubwa kwa jamii. Alisema hayo Ijumaa iliyopita.
Senata Ron Johnson wa Wisconsin pia alionesha nia ya kuupinga mpango huo na hivyo kutoa dalili za kushindwa kwa muswada huo unaotarajiw akujadiliwa leo au kesho katika ngazi za kanuni za kawaida.
 “Ni kitu kibaya kabisa kupitisha muswada mbaya kuliko kutoupitisha kabisa,” alisema Paul akizungumza na waandishi wa habari.
Collins yeye aliandika katika twita kwamba alitaka kushirikiana na wenzake kuhakikisha wanaziba maeneo yaliyo na matatizo katika sheria ya kwanza lakini hii ya sasa haina mwanya huo.

Kwa muda wa miaka saba TRepublican awamekuwa wakijaribu kuondoa alama muhimu ya kihistoria katika skimu za afya za Marekani iliyofanywa na Rais barack Obama kwa ajili ya watu maskini.
Source: The New York Times

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO