KAMANDA wa Polisi mkoa wa Ruvuma, Gemini Mushy amekemea vitendo vinavyofanywa na madereva wa bodaboda ikiwemo kushiriki vitendo vya ujambazi.

Aidha alisema kwamba pamoja na ushiriki wao huo tabia wanayofanya ya kukimbia baada ya kusababisha ajali,pamoja na kuwanyanyasa kijinsia wanawake ikiwamo kubaka vinaondoa heshima yausafiri huo na kuufanya kuwa wa shaka.

Pamoja na kukemea matendo hayo kamanda huyo  amewataka wanaoshiriki kuacha mara moja na wananchi pamoja na waendesha pikipiki wenye nia njema kuwaripoti watenda maovu hayo.

Alisema serikali imeruhusu usafiri wa bodaboda kwa nia njema kabisa kwa lengo la kurahisisha masuala ya usafiri na kutoa kipato lakini haivumilii matumizi maovu ya vyombo hivyo.

“Nataka kusema yeyote atakaye mwona mwenzake akifanya viendo vya kinyama au kushiriki ujambazi basi mara moja atoe tarifa kwa jeshi la polisi ili hatua kali za kisheria zichukuliwe” alisema kamanda huyo.

Kamanda Mushi alisema hayo wakati akijitambulisha kwa waendesha bodaboda mkoani Ruvuma.

Aidha aliwataka kuepusha ajali za barabarani zinazosababishwa na wao kutozingatia sheria za usalama barabarani ikiwamo ya mwendo kasi.

Kamanda huyo amewataka madereva hao kuacha kushiriki katika msoroborika (kutaka sifa zisizo na msingi) na kufuata taratibu ili kuwa na usalama wa kutosha kwao na kwa abiria wao.

Wakijibu hoja za kamanda Mushi, waendesha boda boda hao wamesema tatizo si kutoa taareifa bali usalama utakaokuwepo baada ya wao kutoa taarifa husika.

Waendesha bodaboda haow alifafanua kwamba wao hawataki kushiriki vitendo vya ujambazi wala unyanyasaji lakini  wanashindwa sehemu ya kuaminika ya kutoa taarifa kwa kuwa wanapokwenda kutoa taarifa mapokeo huwa kinyume.

Wamehakikishia kamanda huyo kwamba watahakikisha wanafuata sheria za usalama barabarani na kuhakikisha kwamba vitendo vya kihalifu vinadhibitiwa kwa kushirikiana na Polisi.

Wakati huo huo Kamanda Mushi amewataka madereva wa bodaboda kukata bimaya afya ili kuwasaidia katika matatizo ya magonjwa na ajali.
Source:Nindi Mzuza, Songea


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO