New York City - Julai 3, 2017 —MSHIBNDI wa Big Brother Africa w amwaka 2014 Idris Sultan amepata nafasi ya kuigiza katika filamu ya Kimarekani ya ‘Ballin...On the Other Side of the World,' itakayoongozwa na Harvey White, darekta wa muziki mmarekani ambaye amabedilisha fani na kuwa darekta wa filamu.Direkta huyu ameshawahi kufanyakazi na akina Chris Brown, Mariah Carey, Lady Gaga na Tamia.kama mhariri wa sinema alifanyiakazi vitu kama 'Think Like A Man 2,' 'The Wedding Ringer,' na ‘King of The Dance Hall,’ akiwa na Whoopi Goldberg.
Ikiwa imeandikwa na Torino Von Jones, simulizi linamhusu mvulana wa Kikenya (Kunjani), ambaye anakumbana na fadhaa kubwa kutokana an wazazi wake kuwa waathirika wa vurugu za jinai.Siku moja akiwa katika maeneo ya shule akicheza mpira wa kikapu kijana huyo wa miaka 13 anaonwa na padre wa Kimarekani ambaye anaamini kwamba kijana huyu ana fursa katika mpira wa kikapu wa kulipwa NBA.Wawili hao waanzisha urafiki na kuanza kujengana. Lakini maendeleo hayo yanakuwa kinyume na anachotaka (King) nafasi inayochezwa na Sultan.King akiwa kijana mwenye tabasamu daima ni mkuu wa genge la uhalifu na anamtaka Kunjani kw amalengo ya kumwingiza katika kundi la uhalifu. Na kwa namna ilivyo hakuna kitu cha kumzuia.
Mtendaji Mkuu wa D Street na projuza mtendaji Dexter Davis alimjua Idris kupitia filamu ya Kiumeni na kuona kwamba anafaa kwa nafasi za muigizaji kinara.
Filamu hiyo itashutiwa New York na mji mwingine wa Afrika na bajeti yake itakuwa dola milioni


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO