DEKALB COUNTY, Ga

MWIZI maarufu wa vito nchini Marekani, Doris Payne (86) ambaye katika kipindi cha miongo sita iliyopita alifanikiwa kuiba vito vyenye thamani ya dola za Marekani  milioni 2, amedakwa tena lakini sasa kwa kuiba bidhaa mbalimbali zenye thamani ya dola za Marekani 86.22.

Kikongwe huyo ambaye hajawahi kuficha tabia yake ya wizi ameshatumikia miaka kadha jela na kuachwa.

Bidhaa hizo ameiba kutoka duka la Walmart lililopo barabara ya Chamblee Tucker huko DeKalb County.

Payne ameshawahi kutengenezewa filamu inayoelezea maisha yake na uhalifu alioufanya, inayoitwa “The Life and Crimes of Doris Payne.”
Polisi kwa mujibu wa Channel 2 Action News, waliitwa majira ya saa 11 jioni kumkamata mwanamke ambaye alikuwa anaiba vitu katika duka kuu hilo.

Polisi walimnasa mwanamke huyo ambaye baadaye katika kumbukumbu alitambuliwa ndiye Payne akiwa amesunda vifaa vya tiba na elektroniki.
annet

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO