RAISI John Magufuli amesema kuwa ataifunga migodi ya madini nchini iwapo wawekezaji watachelewa kufanya mazungumzo na ya kurejesha fedha walizochuka kutokana na udanganyifu walioufanya katika kusafirisha nje mchanga Wa madini maarufu kama makinikia.

Akizungumza wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi Wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Nyakazi wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera hadi Kakonko mkoani Kigoma alisema kuwa anasubiri wawekezaji hao waje kwenye mazungumzo lakini muda ukizidi mazungumzo hayatakuwepo na migodi itafungwa.

Raisi Magufuli alisema  kuwa vinginevyo ni bora migodi igawanywe kwa Watanzania wazalendo wachimbe wenyewe wauze na kulipa kodi.

Alisema kuwa wamekuja wawekezaji wakachimba madini na kuwaibia Watanzania kwa muda mrefu kwamba wanachobeba ni mchanga wakati kuna aina 12 za madini zilizokuwa zikisafirishwa bila kulipiwa kodi.


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO