MKAZI  wa mtaa wa Tambukaleli manispaa ya Shinyanga  Sarah Bundala (55) amekutwa na mume wake  amejinyonga chumbani kwake.
Inaaminika sababu za kujinyonga kwake ni kushindwa kupata fedha kiasi cha shilingi elfu 40 alizomdhamini rafiki yake ambaye ametoroka.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Jumanne Muliro, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba maiti imehifadhiwa mochwari .
Akizungumzia tukio hilo mume wa marehemu Laurent Mabina alisema wakati akiwa bado kazini majira ya saa 9 mchana alipigiwa Simu na mke wake akimuomba Shilingi 40,000.
Alimwambia kwamba kwa kuwa anarejea nyumbani wataangalia cha kufanya lakini alipofika akakuta mkewe amejinyonga.
Alisema katika kuhangaika ndipo aliambiwa kwamba mke wake alijinyonga kwa kuwa anadaiwa.
Alisema kwamba mkewe alishawahi kukopa fedha akashindwa nay eye akalazimika kulipa na kumuonya kwamba asikope tena.

”Sababu ya  mke wangu   kujinyonga, nadhani ni ile hofu kuwa nikirudi nyumbani nitakuja kugombana naye sababu nilishamkataza kujiingiza kwenye masuala ya mikopo,”alisema Mabina.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO