JUNI 28 Supamodo Rosie Huntington-Whiteley  amejifungua mtoto wake wa kwanza aliyezaa na mchumba wake muigizaji mbabe na mwanakareteka Jason Statham.

Mdada huyo alitangaza ujio wa mtoto wake wa kwanza kupitia  Instagram  katika posti yake ya Jumatano Juni  28.

"Mtoto wetu amewasili Jumamosi Juni 24! Jack Oscar Statham  akiwa na paundi 8.8," alisea katika kapsheni kwenye picha inayoonesha mkono wake tu mtoto.


Wawili hao ambao walianza mapenzi wakati wakiwa katika uchukuaji wa picha za Transformers mwaka 2011, Februari mwaka huu walitangaza kwamba wanatarajia kupata mtoto  baadae mwaka huu.

“Ninafurahi sana kusema kwamba mimi Na jason tunatarajia mtoto wetu!” alisema wakati huo na kuongeza  kwamab tunawapenda sana.


Kama ilivyoripotiwa awali  kwamba mwamba huyo wa Furious 7  mwenye umri wa miaka, 49, aliomba mkono wa uchumba Januari 2016 miaka mitano baada ya kuanza kukutana. Baadae kidogo mrimbwende huyo wa kiingereza alivishwa pete ya karati tano yenye thamani ya dola za Marekani 350,000.

Pete hiyo ni dizaini ya  Neil Lane na alivikwa wakatimwa red carpet mwaka jana kwenye tuzo za Golden Globe.

Mrimbwende huyo wa Victoria’s Secret  alisema Aprili 2015 kwamba kunakuwa na shinikizo kubwa la ndoa kwa watu walioishi pamoja kwa muda, lakini yeye pamoja na kuamini katika taasisi ya ndoa lakini kitendo cha kuwa katima uhusiano wenye furaha ni kitu muhimu sana kwake.

"Sisi ni marafiki wazuri sana," aliendelea kusema. “ Hunifanya nicheke kila siku mpaka  najiona kama vile sijawahi kuwa na rafiki wa kiume kabla!”

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO