Mwanamuziki mkongwe Shaaban Dede amefariki dunia leo saa mbili asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu
kwa takriban wiki mbili, mwanae Hamad Dede amethibitisha.

Hamad Dede amesema mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Mbagala jijini Dar es salaam, na kwamba ratiba na taratibu zote zitatangazwa mara zitapokamilika kupangwa.

Marehemu Dede atakumbukwa kama mmoja wa wanamuziki nguli kutokea nchini Tanzania kwa sauti yake tamu na utunzi wa nyimbo mbalimbali zilizoshika
chati akiwa na bendi mbalimbali zikiwemo Tabora Jazz, Bima Lee, Mlimani Park na Mondo Ngoma ambako alikuwa anatumikia hadi mauti yanamkuta.

Globu ya Jamii inatoa mkono wa rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na mashabiki wa Shaaban  Dede
kwa kuondokewa na mkongwe huyu wa muziki.

Mola aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi - AMIN

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO