Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Hassan Abbas kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari, Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. Hassan Abbas umeanza tarehe 09 Agosti, 2017.
Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Hassan Abbas alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Maelezo na aliteuliwa kushika nafasi hiyo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma namba 8 ya mwaka 2002.
Dkt. Hassan Abbas ameteuliwa kushika nafasi hiyo kwa mujibu wa Sheria Mpya ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016, ambapo nafasi hiyo imebadilishwa kutoka Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Maelezo na kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari, Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali na Mamlaka ya uteuzi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
11 Agosti, 2017

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO