AMINA  Mwesigwa (37) anayesumbuliwa na ugonjwa  unaoathiri mishipa ya fahamu, misuli, moyo na figo (autoimmune motor sensory) au kwa kitaalamu motor sensory polyneuropathy tangu mwaka 2013 anaomba msaada wa matibabu ili aweze kurejea katika hali yake ya kawaida.
Kwa sasa ugonjwa huo umeshaathiri sehemu kubwa ya viungo vyake, ikiwa ni pamoja na kutokunjuka kwa vidole na kufa ganzi na kutoweza kusimama. Aidha kwa sasa hana kazi.
Akizungumza amesema kwamba wataalamu wa kliniki za Muhimbili na Family Care wameshauri kupatiwa dawa aina ya immunoglobulin IV  kwa dozi ya dripu tano, lakini anashindwa kuinunua kutokana na gharama zake.
Amesema kuwa dawa hizo jumla yake  ni Sh milioni 10 na yeye hana uwezo na hivyo kuomba wasamaria kumsaidia  ili aweze kurejea katika hali ya kawaida ili aweze kujisaidia mwenyewe.
Sina uwezo wa kununua hizo dawa naomba msaada kwa yeyote atakayeweza kunichangia niweze kupata hizo dawa.
Naomba mnisaidie ili nami niweze kupona nitembee tena mwenyewe na vidole vyangu vikunjuke niweze kufanya kila kitu na kushika vitu nimeteseka kwa miaka minne na hili tatizo naomba msaada wenu na Mungu awabariki sana, alisema.
Aidha alisema kwamba anayetaka kumsaidia anaweza kuwasiliana naye katika anuani zifuatazo:
Namba ya simu ni : ±255 713 612754 (0713 612754) au kuweka moja kwa moja benki kwa jina la Amina Mwesigwa akaunti namba : 001340468640001 Amana Bank. Pia barua pepe yake ni: emimwesi@gmail.com.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO