MTANDAO MPYA WA VYOMBO VYA HABARI VYA KIJAMII WASAJILIWA NCHINI

Mtandao mpya unaoundwa na Radio na vyombo vya habari vya kijamii Tanzania chini ya shirika la vyombo vya habari vya maudhui ya kijamii ulios...

Mtandao mpya unaoundwa na Radio na vyombo vya habari vya kijamii Tanzania chini ya shirika la vyombo vya habari vya maudhui ya kijamii uliosajiliwa kwa jina la TANZANIA DEVELOPMENT INFORMATION ORGANIZATION-TADIO umeanzishwa rasmi baada ya kuvunjika kwa mtandao wa zamani wa COMNETA. Tukio hilo limetokea Julai 28, 2017 katika mkutano mkuu wa kwanza ambao pamoja na mambo mengine ulichagua safu mpya ya viongozi wa mtandao huo. Shirika la mtandao wa vyombo vya habari jamii Tanzania uliokuwa na jina la COMMUNITY MEDIA NETWORK OF TANZANIA – COMNETA, limevunjika rasmi mwezi machi mwaka huu. Katika mkutano huo kuwa kuundwa kwa shirika hilo jipya kunalenga kuhakikisha kunakuwa na mtandao makini wa Radio na vyombo vingine vilivyojikita katika kuibua kwa kuandika na kutangaza masuala ya kijamii kwa ajili ya maendeleo. [caption id="attachment_2595" align="aligncenter" width="640"] Mwenyekiti mpya wa TADIO, Prosper Kwigize akizungumza jambo na wajumbe wakati wa mkutano huo.[/caption] Akihutubia katika mkutano huu kaimu mkuu wa ofisi ya UNESCO Tanzania, ambao ni wafadhili wakubwa wa mtandao huo Bw. Christophe Legay kwa niaba ya Mkuu wa ofisi Bi. Zulmira Rodrigues amepongeza hatua iliyofikiwa na Radio wanachama ya kuunda mtandao mpya. Alieleza kuwa UNESCO itaendelea kufanya kazi bega kwa bega na shirika hilo jipya la TADIO ili kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata huduma sahihi za kihabari zitakazosaidia kuboresha maisha yao na kuchochea maendeleo ya upashanaji wa habari nchini. Bw. Christophe amehimiza kwamba vyombo vya jamii vinao wajibu mkubwa wa kuhakikisha sauti za watu wanaowahudumia hasa wanaoishi vijijini. [caption id="attachment_2588" align="aligncenter" width="640"] Mwenyekiti mpya waTADIO Bw. Prosper Kwigize akizungumza jambo na wajumbe mara baada ya uchaguzi. Katikati ni mmoja wa wajumbe wa bodi ya TADIO, Maimuna Msangi na Katibu Mtendaji wa TADIO, Marco Mipawa.[/caption] Aliwaasa kushughulika na masuala ya kibinadamu na si watu binafsi. Wakati huo huo Mtandao huo unaoundwa na jumla ya Radio 32 kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Zanzibar, umefanya uchaguzi mkuu na kuwapata viongozi watakaosimamia shughuli zake kwa miaka mitatu ijayo. Uchaguzi huo ulitanguliwa na tukio la kujiuzuru kwa viongozi wa mpito waliochaguliwa mwezi Machi mwaka huu, baada ya kutangazwa rasmi kuvunjika kwa muungano wa awali wa radio jamii wa COMNETA. [caption id="attachment_2589" align="aligncenter" width="640"] Katibu Mtendaji mpya wa TADIO, Marco Mipawa (kulia) akizungumza jambo mara baada ya uchaguzi kufanyika. Kutoka kushoto ni Balozi Mstaafu Mh. Christopher Liundi, Mkuu wa idara ya Mawasiliano na Habari wa UNESCO, Ofisi za Tanzania, Christophe Legay, Mwenyekiti mpya waTADIO Bw. Prosper Kwigize na Mjumbe wa Bodi ya TADIO, Maimuna Msangi.[/caption] Akitangaza matokeo, msimamizi wa uchaguzi huo ambae pia ni mlezi wa ushirika huo, Balozi mstaafu Mheshimiwa Christopher Liundi, alimtangaza Bw. Prosper Kwigize aliyekuwa mgombea pekee kuwa Mwenyekiti mpya baada ya kupata kura za ndiyo 26 kati ya kura 30 zilizopigwa na wajumbe waliohudhuria. Balozi Liundi, pia alimtangaza Bw. Marco Mipawa kuwa Katibu Mtendaji baada ya kupata kura 28 za ndiyo, Aidha Mipawa pia alikuwa mgombea pekee katika uchaguzi huo. Viongozi wengine waliochaguliwa ni pamoja na Mweka Hezina, Shaaban Ali Makame aliepata kura 24 za ndiyo. Pia mkutano huo uliwachagua wajumbe sita wa Bodi ya shirika hilo la TADIO ambao ni Maimuna Msangi kutoka Pangani FM, Gladys Mapeka kutoka Radio Kilosa, Ali Mbarouk Omar kutoka kutoka Klabu ya Waandishi wa Habari wa Pemba (PPC), Ali Khamis kutoka Adhana FM Zanzibar, John Baptist kutoka Dodoma FM na Anthony Masai kutoka Triple A FM. [caption id="attachment_2590" align="aligncenter" width="640"] Balozi mstaafu Mh. Christopher Liundi (kulia) akimpongeza akimpongeza Mwenyekiti mpya wa TADIO, Prosper Kwigize.[/caption] Akizungumza baada ya kutangaza matokea hayo, Balozi Liundi aliitaka safu ya uongozi mpya kuongoza kwa kufuata katiba na malengo ya shirika hilo kwa lengo la kutetea maslahi mapana ya wananchi kwa kupitia kazi zinazofanywa na radio za kijamii. Kwa upande wake, Mwenyekiti mpya wa TADIO Bw. Prosper Kwigize amewashukuru wajumbe kwa kuchagua safu mpya ya uongozi na kuahidi kujenga ushirikiano mpya ambao utawezesha kufikiwa kwa malengo ya kuanzishwa kwa mtandao huo wa ushirikiano wa vyombo vya habari vya kijamii. Bw. Kwigize ametoa wito kwa wadau wengine hususani Radio za kitaifa, magazeti, waandishi wa habari za mitandaoni (bloggers) Muungano wa wamiliki wa vyombo vya habari MOAT, TAMWA, MISA, Baraza la Habari Tanzania, Runinga na Vilabu vya waandishi wa habari mikoani kushirikiana na shirika la TADIO ili kutoa huduma stahiki kwa jamii. [caption id="attachment_2591" align="aligncenter" width="640"] Balozi mstaafu Mh. Christopher Liundi akimpa pongezi Katibu wa TADIO Bw. Marco Mipawa (shati la kitenge) mara baada ya matokeo kutangazwa.[/caption] Amehimiza pia serikali na taasisi zake kutoa ushirikiano kwa TADIO ili misimamo, dira na malengo yanayoibuliwa na serikali yawafikie wananchi kwa haraka kupitia muungano huo wa Radio za mikoani. Amesisitiza kuwa, mtandao huo wa TADIO una ofisi na studio ya kisasa ndani ya Chuo Kikuu Huria Tanzania – OUT makao makuu Kinondoni Dar es Salaam ambako kazi ya ofisi na studio hiyo ni kuratibu shughuli za mtandao pamoja na kuandaa vipindi ambavyo vitakuwa vikisambazwa kwa radio wanachama. Aliitaka safu ya uongozi mpya kuacha kufanya kazi kwa mazoea, kujenga umoja na mshikamano pamoja na kufanya kazi kwa bidii na ubunifu ili kuyafikia malengo ya ushirika huo. Mtandao wa TADIO unafadhiliwa na UNESCO chini ya mradi wa SIDA/SDC. [caption id="attachment_2592" align="aligncenter" width="640"] Msimamizi wa uchaguzi huo mwanasheria Harold Sungusia (mwenye tai) akimpongeza Mwenyekiti mteule wa TADIO, Prosper Kwigize.[/caption] [caption id="attachment_2594" align="aligncenter" width="640"] Picha ya pamoja ya viongozi wa TADIO, Balozi mstaafu Mh. Christopher Liundi na Msimamizi wa uchaguzi huo Mwanasheria Harold Sungusia.[/caption]

COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,302,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4816,habari. dodoma,24,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,sto,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: MTANDAO MPYA WA VYOMBO VYA HABARI VYA KIJAMII WASAJILIWA NCHINI
MTANDAO MPYA WA VYOMBO VYA HABARI VYA KIJAMII WASAJILIWA NCHINI
http://www.thebeauty.co.tz/wp-content/uploads/2017/07/IMG_9004.jpg
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2017/08/mtandao-mpya-wa-vyombo-vya-habari-vya.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2017/08/mtandao-mpya-wa-vyombo-vya-habari-vya.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy