KAMPUNI ya bia nchini ya TBL imepewa tuzo ya kwanza ya matumizi bora ya magari makubwa ya mizigo ya Mercedes Benz Actros ambayo yametimiza zaidi ya kilomita milioni moja huku yakiwa bado katika hali bora. TBL ina magari kumi ya aina hiyo ambayo yamefanya kazi kwa miaka 17. Tuzo hiyo imetolewa na DAIMLER kwa kushirikiana na kampuni tanzu ya CFAO nchini Tanzania ambayo ndiyo mawakala pekee wa magari ya Mercedes Benz nchini Tanzania. Tuzo hiyo Mercedes-Benz Actros yenye kubeba jina la ‘Mileage Millionaire’ kutokana na kupita kilomita milioni moja, imetolewa kuonesha kuridhishwa kwa watengenezaji wa magari hayo juu ya uimara wake. TBL ina magari zaidi ya 80 ya Mercedes Benz. Magari yote hayo yamefikisha kilomita milioni 11 katika miaka 17 ya kuwa barabarani. Kilomita hizo ni sawa na kuzunguka dunia mara 275. [caption id="attachment_3141" align="aligncenter" width="1404"] Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Tanzania, Marius Prinsloo akisalimiana na kuwakaribisha baadhi ya wageni waalikwa waliowasili kwenye hafla ya tuzo ya Mileage Millionaire kwa kampuni ya bia ya TBL. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro.[/caption] Gari linaloongoza katika ‘Mileage Millionaire’ ni Actros modeli ya 3340, ambalo limefikisha kilomita 1,519,459 tangu lilipoingizwa TBL mwaka 2000. Magari mengine ni Actros za mwaka 2002,2003 na 2004 zikiwa na wastani wa kilomita kati ya kilomita milioni 1.02 na 1.5. Magari hayo yamekuwa yakitumika katika njia zote za Tanzania kupeleka vinywaji kutoka Dar es salaam, Arusha na Mwanza kwenda maeneo mbalimbali ya Tanzania. Kwa mujibu wa taarifa magari yote hayo yalinunuliwa moja kwa moja kutoka CFAO Motors Tanzania. Bosi wa magari ya kibiashara ya Daimler upande wa Afrika, Naeem Hassim alisema katika kukabidhi tuzo hizo kwa TBL kwamba kuwa na magari ya aina hiyo katika kampuni yake kufikisha zaidi ya kilomita milioni 1 na bado yakiwa ‘vijana’ si jambo la kushtusha kwa Mercedes-Benz Actros. [caption id="attachment_3142" align="aligncenter" width="1404"] Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa CFAO Motors Tanzania Bi. Tharaia Ahmed (katikati) akifurahi jambo na mmoja wa wageni waalikwa kabla ya kuanza kwa hafla ya utoaji tuzo ya Mileage Millionaire. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Tanzania, Marius Prinsloo na kulia ni Mwakilishi wa CFAO, Simon Faraldo.[/caption] Alisema Actros yamejitanabaisha kwa ubora wake na kuaminika kwake:” ni dhahiri kuwa na magari kama haya ni uwekezaji wenye maana kubwa, ni vyema wateja wakayambua kwamba Actros ni gari la kuaminika.” Naye Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Tanzania, Marius Prinsloo alisema katika utoaji tuzo huo kwamba wanafurahi sana kusherehekea kilomita zaidi ya milioni moja ya magari ya ACTROS. Alisema ni mafanikio makubwa kuwa na magari hayo na hiyo inamaananisha kwamba ni imara na yanayoaminika yakiwa yametengenezwa kuhimili hali mbaya zaidi na kwamba wateja wanaweza wakawategemea kwa huduma bora za mauzo na pia uhudumiaji wa gari lenyewe ili liweze kudumu zaidi. Akipokea tuzo hiyo mwakilishi wa Tanzania Breweries Limited, ambaye ni meneja wa lojistiki wa Afrika Mashariki James Nyoike alisema kwamba amefurahi sana kuwa sehemu ya simulizi lenye mafanikio katika uendeshaji wa kampuni kwa kuwa na magari yenye sifa kubwa wa uimara. [caption id="attachment_3143" align="aligncenter" width="1404"] Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Tanzania, Marius Prinsloo (kushoto) akifafanua jambo kwa mmoja wa wageni waalikwa kwenye hafla ya kuitunuku kampuni ya TBL tuzo ya Mileage Millionaires baada ya magari yake 10 aina ya Mercedes Benz Actros kupitisha kilometa zaidi ya milioni moja na yakiwa bado ni imara. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam katika Hotel ya Hyatt Regency - The Kilimanjaro.[/caption] Alisema anafurahia huduma ya matengenezo inayopata magari yake kila yanapotakiwa kutengenezwa, pamoja na mafunzo kwa madereva hali iliyowezesha kuwapo kwa udumu zaidi kwa magari. “Tuna zaidi ya magari 80 ya Mercedes Benz kuanzia modeli za 2000 hadi 2016. Magari haya yamethibitisha ubora wake kazini na kuwa sehemu muhimu sana ya kazi zetu hasa za usambazaji wa bidhaa” alisema Nyoike. Katika mahojiano alisema kwamba gari lililopitisha kilomita milioni 1.5 T 418 AAT limeendeshwa na dereva mmoja Moses Ulenga kwa miaka 10. “Nasikitika kwamba hakuhudhuria sherehe hizi, yuko safari” alisema Nyoike ambaye alisema pamoja na kufuata utaratibu wa service wa gari pia wamekuwa wakifanyia matengenezo ya kuzuia uharibifu na kwamba madereva wake wamefunzwa na zipo taratibu za kufuata zenye kuonesha nidhamu ya barabara. [caption id="attachment_3152" align="aligncenter" width="1404"] Mgeni rasmi katika hafla ya kuitunuku kampuni ya bia TBL tuzo ya Mileage Millionaires, Meneja Mauzo wa kampuni ya Daimler wa magari ya Mercedes Benz Afrika, Hansjörg Richter (kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya wageni waalikwa kwenye hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro.[/caption] Naye Tharaia Ahmed Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko amesema kwamba wamemua kutoa tuzo hiyo kwa TBL kama sehemu ya kuonesha namna gani ushirikiano kuanzia mauzo hadi matunzo unavyoweza kumnufaisha mtu ambaye ananunua magari hayo kutoka CFAO. Alisema TBL imeonesha ubora wa magari hayo na kuaminika kwake katika safari ambazo wakati mwingine ni ngumu sana kwa kuzingatia mazingira vyetu. CFAO Motors Tanzania ambayo zamani ilijulikana kama DT Dobie ni kampuni tanzu ya kundi la makampuni ya CFAO ya Ufaransa. CFAO Motors iliundwa 1952na ni wakala wa magari mbalimbali Mercedes-Benz ya kibiashara, ya abiria na ya binafsi. [caption id="attachment_3132" align="aligncenter" width="1404"] Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Tanzania, Marius Prinsloo akizungumza katika hafla ya kuitunuku kampuni ya TBL tuzo ya Mileage Millionaire baada ya magari yake 10 aina ya Mercedes Benz kupitisha kilometa zaidi ya milioni moja na yakiwa bado ni imara. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam katika Hotel ya Hyatt Regency - The Kilimanjaro.[/caption] [caption id="attachment_3131" align="aligncenter" width="1404"] Mgeni rasmi katika hafla ya kuitunuku kampuni ya bia TBL tuzo ya Mileage Millionaire, Meneja Mauzo wa kampuni ya Daimler wa magari ya Mercedes Benz Afrika, Hansjörg Richter akizungumzia ubora wa magari ambayo yanauzwa na CFAO Motors na mipango ya kampuni hiyo kuendelea kuuza magari imara kwa mazingira ya Afrika.[/caption] [caption id="attachment_3133" align="aligncenter" width="1404"] Picha ya pamoja kabla ya kukabidhi tuzo ya Mileage Millionaire.[/caption] [caption id="attachment_3134" align="aligncenter" width="1404"] Meneja Mauzo wa kampuni ya Daimler wa magari ya Mercedes Benz Afrika, Hansjörg Richter (wa pili kulia) akimkabidhi tuzo ya Mileage Millionaire mwakilishi wa kampuni ya bia TBL, Denis Dismas (katikati). Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Tanzania, Marius Prinsloo.[/caption] [caption id="attachment_3135" align="aligncenter" width="1404"] Pichani juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa ambao ni wateja wa CFAO Motors Tanzania waliohudhuria hafla hiyo ya kuitunuku kampuni ya bia TBL tuzo ya Mileage Millionaire.[/caption] [caption id="attachment_3153" align="aligncenter" width="1404"] Mgeni rasmi katika hafla ya kuitunuku kampuni ya bia TBL tuzo ya Mileage Millionaires, Meneja Mauzo wa kampuni ya Daimler wa magari ya Mercedes Benz Afrika, Hansjörg Richter (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Tanzania, Marius Prinsloo (kushoto) katika picha ya pamoja na wawakilishi wa kampuni ya bia ya TBL mara baada ya kukabidhi tuzo hiyo.[/caption] [caption id="attachment_3144" align="aligncenter" width="1404"] Picha ya pamoja ya Uongozi wa CFAO Motors Tanzania na ugeni kutoka makao makuu ya kampuni hiyo.[/caption] [caption id="attachment_3145" align="aligncenter" width="1404"] Uongozi wa Kampuni ya CFAO Motors Tanzania na mgeni kutoka DAIMLER katika picha ya pamoja mbele ya gari moja kati ya 10 aina ya Mercedes Benz Actros ya kampuni ya bia ya TBL iliyopitisha kilometa 1,519,459 na kupelekea kukabidhiwa tuzo ya Mileage Millionaire. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro.[/caption] [caption id="attachment_3138" align="aligncenter" width="1404"] Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa CFAO Motors Tanzania Bi. Tharaia Ahmed akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu tuzo ya Mileage Millionaire iliyotolewa na CFAO Motors Tanzania kwa kampuni ya bia TBL.[/caption] [caption id="attachment_3139" align="aligncenter" width="1404"] Mkuu wa (Logistics Services) wa kampuni ya bia TBL, James Nyoike akizungumza na waandishi wa habari namna TBL imefanikiwa kutunza magari yake aina Mercedes Benz Actros na kuweza kufikisha kilometa 1,519,459.[/caption] [caption id="attachment_3140" align="aligncenter" width="1404"] Wawakilishi wa kampuni ya bia TBL, James Nyoike (wa pili kushoto) na Denis Dismas (wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi katika hafla ya kuitunuku kampuni ya bia TBL tuzo ya Mileage Millionaire, Meneja Mauzo wa kampuni ya Daimler wa magari ya Mercedes Benz Afrika, Hansjörg Richter (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Tanzania, Marius Prinsloo (wa kwanza kulia).[/caption]

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO