Waziri wa kazi wa Colombia Rafael Pardo Rueda (kushoto) akipongezana na  Mtendaji wa sjhirika la Umoja wa Mataifa la dawa za kulevya na Uhalifu (UNODC)  Yury Fedotov (kulia) huku Mtendaji wa wakala wa serikali wa ujenzi upya wa maeneo, Mariana Escobar akiangalia.

TAIFA la Colombia limetia saini mkataba wa  dola milioni 300 na Umoja wa Mataifa wenye lengo la kupunguza uzalishaji wa dawa za kulevya aina ya kokeni.
Kwa mujibu wa makubaliano wakulima wataacha kulima zao hilo linalotengeneza dawa za kulevya na kulima mazao mengine ya biashara.
Akizungumza kutoka Vienna, Austria, Mtendaji mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na Uhalifu na Dawa za Kulevya (UNODC), Yury Fedotov amesema hatua hiyo ni fursa ya kuibadili Colombia kufanya shughuli nyingine za uzalishaji na kuachana na mmea wa kokeni.
Pia hatua hiyo itasaidia kupatikana kwa amani kwa kuwa sasa wakulima watajihusisha zaidi na kilimo chenye staha badala ya sasa.
Kwa sasa wakulima kila mwezi hupata dola za Marekani 300 kwa kila ekari ya mmea wa kokeni wanaouzalisha. Fedha zilizotolewa zinatarajiwa kufidia fedha hizo ili wananchi waachane na kilimo hicho.
Hata hivyo, serikali ya Colombia inasema kwamba mpango huo unapata changamoto kubwa kutoka kwa makundi yenye silaha ambayo yananeemeka kwa  zao hilo.
Ijumaa mwaka huu  Umoja wa Mataifa umesema kumekuwepo ongezeko la asilimia 50 la  eneo ambalo linaendesha kilimo hicho.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO