MWANDISHI wa habari mkongwe nchini aliyewahi kufanya kazi katika vyombo mbalimbali maarufu vya habari nchini ikiwemo gazeti la Daily News, Abdallah Yakuti, amefariki dunia.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na familia ya Yakuti ilisema mwandishi huyo wa habari mkongwe alifariki dunia mchana leo katika Hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es Salaam.
Taarifa hiyo ilisema msiba  upo nyumbani kwa marehemu Mabibo jijini Dar es Salaam na kwamba mazishi yamepangwa kufanyika  Ijumaa baada ya Swalat ya Adhuhuri.
Yakuti  ambaye hadi anastaafu kazi ya uandishi wa habari alikuwa mfanyakazi wa Shirika la Magazeti ya Serikali (TSN)  alikuwa Mkuu wa Kituo cha Zanzibar  kwa miaka mingi kabla ya kurudi jijini Dar es Salaam baadaye.
Menejimenti ya Shirika la Magazeti ya Serikali imetoa salamu za rambirambi kwa ndugu na jamaa wa marehemu Yakuti kutokana na msiba huo.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO