Nimemalizia mwaka kwa kuangalia filamu za kibongo nne; Nazo ni Father Ezra, Fitina Dhidi yangu, Nabii Mswahili na Why.
Ukiingalia filamu ya Father Ezra katika nchi ambayo makanisa mapya yanayochipuka kila kukicha kwa kasi unaweza kupata fadhaa amabyo mtengeneza sinema hii anayo.
Sinema hii imegonganisha kwa kiwango kikubwa mawazo ndani ya kitabu husika, kwa kuonesha watu wanavyokosa subira na kubaki kusubiri kupata muujiza.
Lakini labda nawe umeiona filamu hii, kwa namna yako nikuulize weye kama mtaalamu wa kutazama sinema na unayejua falsafa za filamu na maudhui yake katika jamii inayoamini sana dini zake. Filamu ya Father Ezra umeionaje?
Nimekuuliza ili urejee katika mahangaiko yako na utambue kwamba kutengeneza shari ni lazima uwe na sababu na kuitafuta heri ni lazima uwe na sababu.
Simulizi lake limejikita na kwa namna ambavyo jamii inapotoka na kuamini katika muujiza na mali na hivyo kuabudu baali badala ya Mungu wa kweli. Hiki ni kizazi cha nyoka ni kizazi cha Miujiza .
Hili si swali lakini niulize kuwapo kwa uwingi wa makanisa ya kisasa yanayotangaza ushuhuda wa mali hili haliwezi kuwa tatizo?
Sina tatizo nayo  kiprofesheno kwani naamini  imetengenezwa katika hali ya kuangalia makandokando ya  imani zetu za kisasa kutokana alivyosimulia na alivyojenga visa vyake akihimiza zaidi kutambua ukweli kwa macho na kupambana na uwongo wake ka nguvu zote ukitambua kwamba huenda ni wewe peke yako unayejua.
Filamu hii ina matatizo nya kihariri na hata upigaji picha wake, rangi yake kama iliyohbabuka inaashiria mengi zaidi. Filamu hii kwenye thieta inaweza isifiti kabisa.
Pia namna alivyoingiza wahusika wenye miliki za ajabu katika njia ambayo ni rahisi mno, kama mtu anayechunguza wakati kam a isivyojulikana mashetani yaliyobeba sura za binadamu yanatokeas wapi angefanya hivyo lakini si kama anajifunza wakati yeye ni gwiji.
Pia namna ambavyo pete yake inatumika unatakiw akuwa maarifa ya kuangalia na kuna sehemu effects zingetumika zaidi kuonesha nguvu ya pete sivyo mtu wa kawaida hawezi kuunga maneno na vitendo.
Mbaya zaidi inaonekana kanisa zima limepegawa na kuvutwa upande wa shetani.
Mbaya zaidi kama mtu hujaiona hii ni namna vipande vya ubakaji vilivyowekwa, vipande hivi vinaashiria wazi kwamba sinema hii watoto hawastahili kuiona, fikira zimepelekwa wazi sana.
Mwanga na sauti katika sinema hii si sawa ni kama vile mtu kaona sinema za ulaya zinaozhusu waabuduo  miungu na kuijaribisha akikwepa kukamatwa.
Lakini inamaliza kwa maneno ya kukuambia na kukuonesha kwamba kanisa hili na wafuasi wake wanaongezeka kwani kundi lililoibuliwa limepwa nyenzo za kwenda kutengeneza wafuasi wao wengine  si wanapenda miujiza?
Inaweza kuwa chungu kumeza kwa watu waliopitiliza imani lakini ndio ukweli unaobeba na maneno ya maandiko kwamba kizazi cha nyoka kinataka ishara na miujiza badala ya kweli na subira.
Fitina dhidi yangu
Sinema hii ilistahili kubadilishwa jina kwani hili la sasa lina walakini kutokana na asilimia 75 kuwa gubu la mke kabisa dhidi ya mkwe sasa hii fitina ipo asilimia ndogo tu na mwisho wake ni mwepesi kwa imani yangu mimi.
Mwepesi kwa kuwa mambo mazito yamefikiwa conclusion kwa sekunde chache tu tena kirahisi rahisi kama utamaduni wa kizungu wakati waswahili ni vuta nkuvute.
WHY
Why ni Bongo movies pamoja na  viashiria vya mwanzo kuwa katika sinema kubwa za Ulaya kwa kuonesha ndege nyingi angani, kuonesha nini kimo ndani ya sinema, simulizi hili ndani unafungua na ndege na kumalizia na pingu.
Kiasi fulani simulizi la mapenzi lililoenda kombo kwa uwongo, uzandiki,ukahaba na subira dhaifu ya kudonoa ukweli na kasha bahati mbaya ya kupitiliza wakati wa urekebishaji wa mambo. Kama ilivyo sinema yenyewe Kwanini (WHY) unaweza kubaini maswali mengi mno. Kuna swali katika mapenzi, kuna swali katika maisha, kuna swali katika undugu, kuna swali katikia kuokoa maisha na kuna swali katika haki za binadamu. Mbaya zaidi suala kwanini kuwapo kwa kichefuchefu cha roho mbaya, uwongo na usaliti.
Tunu (Jennifer) aliwakilisha vyema nafasi yake ya maumivu ya upenzi na upendo kiasi ya kwamba unaiona wazi katika sura yake na miondoko yake japo ana mistari michache zaidi katika sinema hii.
Shamsa Ford yumo katika sinema hii kwani yeye ndiye aliyesababisha Jamal kupata wazimu baada ya kufa mikononi mwake wakati akitaka  kumzuia.
Kuna baadhi ya sehemu zinasisimua lakini namna walivyomtaka Jamal awe kichaa nadhani kunakosa la maandiko twisti za stori  haionekani wazi.
Nabii Mswahili
Katika sinema hizi nne  nilizoangalia mwishoni mwa mwaka  hii ndiyo my favourite. Imetoka kabisa katika sinema tulizozoea naiona kama Feature lakini wahusika wake katika visa vidogo vidogo wamejenga hisia katika maisha ya kawaida yenye kujali wastani na kiasi.
Kichaa ambaye kwangu mimi kama mjulimlisha hoja na mtoa hoja kuu,anawakilisha taifa lenye makunyanzi mengi katika maleba iliyojivika, ikiwa na busara lakini haiaminiki. Simulizi lake japo liko na vipande hadithi imeungwa kutazama uhalisia wa maisha katika jamii, mitafaruku katika rushwa kubwa na ndogo na wajibu wa kila mwanakaya kutunza mazingira yake kuwa safi kuanzia kichwani(akili) nyumbani anavyoongoza kaya na jinsi anavyoopokea shauri mbalimbali.,
Hayo ni machache niliyoyaona  ambayo nilitaka kushea nawe wakati tunamalizia mwaka, mwakani tutakuwa sana na review na critique mbalimbali za sinema za hapa nyumbani.
Katika sinema nimesema nimeipenda Nabii Mswahili na humu ndani kuna maeneo mawili ya suspense ambayo yanakufanya usisimke  bila kuona. Moja ni wakati baba anamchapoa mwanawe anavyotoka kumtandika,fmbo ilivyochakaa na alivyofura kwa hasira na mauaji ya ustaadhi ambapo  mtu anatoka amejaa damu na kutimka, haitoshi kusimulia jinsi darekta alivyoskoa hapa.
Pia kwenye close up za Why,  Tunu ameshaini sana, ameshika nafasi yake ya maumivu vyema kabisa. Unayeangalia unayaona yale maumivu,maumivu ya kupenda na kuona unachopenda kinaharibika.
Tchao
Naitwa Beda Msimbe nikiwa hapa kwetu Goba


Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO