KANISA LA UKOMBOZI LATEMBELEA AMANI, LAKUMBUSHA KUJALI WATOTO

WATANZANIA wamekumbushwa kuwajali na kuwangaalia watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwatimizia mahitaji yao ya ki...

WATANZANIA wamekumbushwa kuwajali na kuwangaalia watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwatimizia mahitaji yao ya kimwili na kiroho. Aidha, wamepaswa kutambua kwamba wana wajibu wa kusaidia watoto hao kwa kuwa wanawekeza kwa manufaa ya taifa na wao wenyewe. Kauli hiyo imetolewa na Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam, akizungumza baada ya kukabidhi vifaa, bidhaa na mahitaji mbalimbali ya watoto yatima wa kituo cha Amani, kilichopo Bagamoyo, kiasi cha kilomita 65 kutoka Dar es salaam. [caption id="attachment_3422" align="aligncenter" width="1404"] na Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko (mwenye gauni la bluu) wa Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam akizungumza jambo mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za Mkurugenzi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Amani, Margareth Mwegalawa (katikati) kukabidhi vitu mbalimbali kituoni hapo akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa kanisa, waumini na wamama.[/caption] Akitoa maneno yanayogusa nyoyo huku akikariri maandiko Mchungaji Faith alisema:“Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu baba ni hii, kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa” Alifafanua kwamba Kanisa lisiloangalia yatima na wajane si Kanisa, alisema na kuongeza kuwa waumini wanastahili kuwajibika kwa hilo. Aidha, alisema kama Kanisa wanajali watoto na ndio maana wamefunga safari kwenda kuwaona na wamefurahi kuwaona na kushiriki nao tafrija fupi baada ya kuwakabidhi zawadi mbalimbali. [caption id="attachment_3423" align="aligncenter" width="1404"] na Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko (wa kwanza kulia) wa Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam na baadhi ya viongozi, wakinamama na waumini wakifungua tafrija hiyo fupi kwa maombi kabla ya kukabidhi mahitaji mbalimbali katika kituo cha kulelea watoto yatima kilichopo kijiji cha Zinga, Bagamoyo.[/caption] Waumini wa kanisa hilo walikabidhi mahitaji ya shule ya watoto, mavazi na chakula. Aliwataka watanzania kuwa na tabia ya kujali watoto hao kwa kuhakikisha wanapata mahitaji yao kila siku na sio siku ya sikukuu tu. Alisema watoaji wanapaswa kutoa kwa hali na mali kwa ajili ya kuondoa dhiki za watoto hao, ikiwa ni sehemu ya Baraka kamili kwa Mungu na pia kwa taifa. Alisema watoto hao hawajulikani kesho watakuwa watu gani na kama watalelewa vyema watakuwa ni sehemu ya taifa lenye uadilifu na woga kwa Mungu. [caption id="attachment_3424" align="aligncenter" width="1404"] Baadhi ya wakinamama wa kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam wakishiriki maombi baada ya kuwasili kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha Amani kilichopo katika kijiji cha Zinga, mjini Bagamoyo.[/caption] Alisema kwa kuwezesha utulivu wa watoto hao, watoto watamjua Mungu na hivyo kujenga taifa lenye maisha yenye utukufu wa Mungu. Naye, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Esther Pilila alisema kwamba kama wanawake katika Kanisa lao wamesukumwa na haja ya kuwaangalia watoto hao kama wajibu wao. Akizungumza kushukuru Mkurugenzi wa kituo hicho Margareth Mwegalawa aliomba watanzania kuwakumbuka watoto hao na kuitafadhalisha serikali kuwapitia kila mara kwa kuwa wao ndio walezi wa watoto. [caption id="attachment_3425" align="aligncenter" width="1404"] Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam akisaini daftari la wageni alipowasili katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Amani kilichopo katika kijiji cha Zinga, Bagamoyo.[/caption] Alisema pamoja na chakula walichopewa wanatamani watu mbalimbali kuendelea kuwajali watoto kwa kuhakikisha wanakuwa salama. Alisema wadau mbalimbali wasiangalie tu vituo vya mashirika ya dini bali vituo vyote ambavyo vinabeba mzigo wa malezi kwa watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi. Alisema kituo cha Amani chenye watoto 40 kinahitaji kupata uzio ili kuhakikisha watoto wapo salama. [caption id="attachment_3426" align="aligncenter" width="1404"] Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam akiwa amempakata mtoto Nicolaus (1.5) wakati wakitazama burudani kutoka kwa watoto wa kituo cha kulelea yatima cha Amani kilichopo katika kijiji cha Zinga, Bagamoyo.[/caption] Naye mtoto Salama Ismail (12) alishukuru kwa misaada hiyo ya mavazi na chakula, mafuta ya kupakaa, miswaki na madaftari na kutaka wananchi wamjue Mungu kwa kuwajali. Naye Haji Joseph (11) aliomba viongozi wa serikali kuwatembelea kwani wao ndio wazazi wao na kuwasaidia kuimarisha upatinakaji wa nishati katika kituo chao hasa umeme wa REA. “Tunaomba viongozi wa serikali watutembelee tuwajue na hasa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa” alisema mtoto huyo. [caption id="attachment_3427" align="aligncenter" width="1404"] Watoto wa kituo cha kulelea yatima cha Amani kilichopo Zinga, Bagamoyo wakitoa burudani sambamba na Mkurugenzi wa kituo hicho Margareth Mwegalawa walipotembelewa na waumini wa kanisa la Ukombozi wakiongozwa na Mchungaji Faith Tetemeko (hawapo pichani) wakati wa tafrija fupi ya kukabidhiwa mahitaji mbalimbali ya kujikumu kituoni hapo.[/caption] [caption id="attachment_3447" align="aligncenter" width="1404"] Pichani juu na chini ni baadhi ya wakinamama wa kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam walioshiriki tafrija hiyo.[/caption] [caption id="attachment_3428" align="aligncenter" width="1404"] Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko (mwenye gauni la bluu) wa Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam akicheza sambamba na mtoto Haji Joseph (11) katika tafrija fupi ambapo Kanisa la Ukombozi lilikabidhi vitu mbalimbali zikiwemo sare za shule, vyakula, madaftari, nguo na mahitaji mengine ya kujikimu.[/caption] [caption id="attachment_3429" align="aligncenter" width="1404"] Pichani juu na chini ni wakinamama wa kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam wakiwa wamebeba vitu mbalimbali vilivyotolewa kwenye kituo cha watoto yatima cha Amani kilichopo Zinga, Bagamoyo.[/caption] [caption id="attachment_3432" align="aligncenter" width="1404"] Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko (katikati) wa Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam akikabidhi vifaa, bidhaa na mahitaji mbalimbali ya watoto wa kituo cha Amani cha watoto yatima, kilichopo Bagamoyo kwa Mkurugenzi wa kituo hicho Bi. Margareth Mwegalawa (kulia) katika hafla fupi iliyofanyika kituoni hapo Bagamoyo. Kushoto ni , Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Kanisa la Ukombozi tawil la Dar es Salaam, Esther Pilila.[/caption] [caption id="attachment_3433" align="aligncenter" width="1404"] Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa kanisa hilo, watoto pamoja na walezi wa kituo hicho.[/caption] [caption id="attachment_3434" align="aligncenter" width="1404"] Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam katika picha ya pamoja na wakinamama wa kanisa hilo na walezi wa kituo hicho mara baada ya kukabidhi msaada huo.[/caption] [caption id="attachment_3435" align="aligncenter" width="1404"] Mwalimu Heavenlight (kushoto) na Mwanaukombozi Favour wakipozi na mtoto Nicolaus (1.5) kuonyesha upendo kwa mtoto huyo.[/caption] [caption id="attachment_3436" align="aligncenter" width="1404"] Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam akigawa chakula kwa watoto yatima wa kituo cha Amani kilichopo Bagamoyo mara baada ya kukabidhi vitu mbalimbali kituo hapo.[/caption] [caption id="attachment_3437" align="aligncenter" width="1404"] Watoto yatima wa kituo cha Amani kilichopo Bagamoyo wakifurahia chakula cha pamoja kilichoandaliwa na wakinamama wa kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_3438" align="aligncenter" width="1404"] Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam akishiriki chakula cha pamoja na watoto yatima wa kituo cha Amani kilichopo Bagamoyo.[/caption] [caption id="attachment_3439" align="aligncenter" width="1404"] Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam akimlisha chakula mmoja wa watoto yatima wa kituo cha Amani kilichopo Bagamoyo mara baada zoezi la kukabidhi misaada mbalimbali kituoni hapo.[/caption] [caption id="attachment_3440" align="aligncenter" width="1404"] Pichani juu na chini ni Wakinamama wa kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam wakicheza michezo mbalimbali na watoto yatima wa kituo cha Amani ukiwemo 'Tulinge Baiyoyo' mchezo ambao katika makuzi kila mtu aliupitia.[/caption] [caption id="attachment_3446" align="aligncenter" width="1404"] Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam, Esther Pilila akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa kituo hicho mara baada ya kuhitimisha zoezi la kukabidhi msaada huo.[/caption] [caption id="attachment_3442" align="aligncenter" width="1404"] Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam akizungumza na kituo cha televisheni cha Channel Ten mara baada ya kukabidhi misaada hiyo kituoni hapo.[/caption] [caption id="attachment_3443" align="aligncenter" width="1406"] Mtoto Haji Joseph (11) wa kituo cha watoto yatima Amani akitoa neno la shukrani kwa kanisa la Ukombozi kwa kupokea misaada hiyo katika tafrija fupi iliyofanyika kituoni hapo.[/caption] [caption id="attachment_3444" align="aligncenter" width="1404"] Mtoto Salama Ismail (12) wa kituo cha watoto yatima cha Amani akitoa shukrani kwa misaada hiyo ya mavazi na chakula, mafuta ya kupakaa, miswaki na madaftari iliyotolewa na wakinamama wa kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_3445" align="aligncenter" width="1404"] Mkurugenzi wa kituo cha watoto yatima cha Amani kilichopo Bagamoyo, Bi. Margareth Mwegalawa akisisitiza jambo wakati wa mahojiano na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kupokea msaada huo.[/caption]

COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,301,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4810,habari. dodoma,23,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: KANISA LA UKOMBOZI LATEMBELEA AMANI, LAKUMBUSHA KUJALI WATOTO
KANISA LA UKOMBOZI LATEMBELEA AMANI, LAKUMBUSHA KUJALI WATOTO
http://www.thebeauty.co.tz/wp-content/uploads/2017/12/JP5A5177.jpg
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2017/12/kanisa-la-ukombozi-latembelea-amani.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2017/12/kanisa-la-ukombozi-latembelea-amani.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy