TAARIFA KWA UMMA
KUSIMAMISHWA KAZI MKURUGENZI MKUU WA NHC
Dodoma, Desemba 16, 2017:

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi kwa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu F. 35 (1) cha Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2009 amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Bw. Nehemia Mchechu.

Aidha, Waziri Lukuvi ameiagiza Bodi ya Shirika hilo kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Huduma za Mikoa na Utawala, Bw. Raymond Mndolwa. Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Dorothy S. Mwanyika, imesisitiza kuwa uamuzi huo unapaswa kutekelezwa kuanzia leo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili watendaji hao.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO