UNAPOSOMA hii makala ama ni siku moja kabla ya krismasi au kama upo pembezoni itakuwa krismasi imepita na unahesabu zawadi walizokuletea, yote heri tu.

Lakini leo katika simulizi zetu za picha nakuletea maelezo mafupi san aya filamu yenye utata ambayo katika mksimu huu wa krismasi itaoneshwa kat6ika majumba machache yaliyochaguliwa.

Usiulize kwanini, huenda hata majumba yetuj nchini moja likaonesha nani anajua?

Wengi wa wachambuzi  wanakubaliana kwamba Phantom Thread ni kitu na boksi ikiwa imetengenezwa vyema kukidhi soko la msimu wa sikukuu na kutopa ujumbe wa msingi kuhusu maisha. Kwanini mpaka uzee wako haujaoa, umejiozesha katika kazi mali na fedha na unadhani ndiyo hayo.

Naam unadhani ndiyo hayo mpaka hapo utakapofunuliwa kwamba kumbe maishja pamoja na yote hayo ni familia, huo ndio naweza kusema ndio ujumbe wa krisma si uliomo ndani ya filamu hiyo yenye dharuba kubwa.

Ikiw aimesukjwa vyema sinema hii inakufanya usisimukwe kwa vicheko vyake kiasi cha kukulewesha kw akuangalia jinsi masuala ya mapenzi yanavyooanza kwa aibu na kuchemka lakini juu ya yote hayo ni namna muigizaji wetu mkuu Daniel Day-Lewis alivyoinogesha sinema hii.
Ikiwa imesukwa katika miaka ya 1950 mjini London, hii ni baada ya vita kuu ya pili ya dunia, mshoni wa nguo Reynolds Woodcock (Daniel Day-Lewis) na dada yake Cyril (Lesley Manville) wanakuw amashuhuri katika suala la fasheni, wakiwavisha watu mashuhuri kama wacheza sinema,warithi, wale wanaojitanabaisha na maisha ya  kujitanua majuu na wengine wenghi waliotaka kujitambulisha na mavazi ya The House of Woodcock.

Wanawakje wanaingia na kutoka katika maisha ya Woodcock,wakiwa kama washiriki tu katika maisha yake. Lakini  alirftika mwanamke, Alma (Vicky Krieps),ambaye alibadili maisha yake akawa ndiye tafakari yake na mpenzi .

Woodcock ambaye alikuw ana maisha yaliyojidhibiti yalisyosukwa vyema baada ya kuingia kwa mwali huyu akabadilika na ndipo anapomshutumu inakuaje hasa kwani toka atokee anaonekana amevuruga maisha yake.

Mwenye filamu hii, Paul Thomas Anderson , ana jambo zito anataka kueleza jamii, anakuchukua vyema katika ubunifu wa kisanii wa mtu huyu ambaye wananwake wanafanya dunia yake iendelee kuwapo.

Phantom Thread  ni sinema ya nane ya Paul Thomas Anderson nan i ya pili akishirikiana na Daniel Day-Lewis.

Ikiwa imetengewa daraja R kutokana na lugha yake yenye mihemuko ya mapenzi na mhhh sinema hii ambayo ni drama itaanza kuonekana Desemba 25 kwa majumba machache.
Muigizaji huyu ambaye  amekuw amshindi wa tuzo ya Oscar mara tatu hivi karibuni alitangaza kustaafu kuigiza na huenda hii ndio picha yake ya mwisho au za mwisho na ameifanya vyema.
Na kama hii itakuwa ya mwisho ya ushoni hakika imejaa , imeshiba na inaweza kuwa raha tupu ukiangalia historia.
Mwanamke huyo aliyempata , alimpata katika mgahawa mhuduu ndani ya mgahawa, alikuwa kama sanamu ya kuchonga kw akupendeza kwake
Poamoja na ukimya wake, mwanamke huyu hakuwa ‘zombi’ wala mjinga na mpumbavu kwani mara tu alipoingizwa katika kumi na nane, alifunga magoli na jamaa akabadilika.
Washoni hupenda kuwa kimya wakishughulikia fani yao kw akufikiri na kjutafakari kuhusu michoro na nini kinapoendea kwa watu. Na ukifanya vurugu kidogo tu mambo yanaharibika.
Moja ya utamu wa sinema hii ni namna unavyolazimika sekunde kadhaa kusubiri  mlipuko wa kukufanya wewe unese katika kiti kwa mshangao au kicheko.
Ni moja ya filamu yenye kufurahisha kujaza mshangao na yenye kumtafadhalisha mtu kuangalia na upande wa pili na sio kazi tu mpaka inakuwa basi tena.
Ni muungano wa ubunifu wa hali ya juu na utendaji uliotukuka katika kazi na maisha ya familia na haja ya kuwa na ‘break’ wakati Fulani.
Kwa muigizaji ninampa heko sana kutokana na jinsi  ilivyokuw ainachomoka na kuingia sindano ya mapenzi na kumfanya  asiwe Yule wa kawaida huku mdada nikimpa ‘dole’ kwa namna alivyotufanya tuwe na sababu ya kuangalia sinema.
Kutoka huku Goba kwa John Luwanda nawatakia  mapumziko mema ya Krismas na mwaka mpya na pasi shaka Mungu atawajalia mema matupu. Mimi bado napatikana katika sms 0713176669 na msimbebeda@gmail.com
mwisho

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO