POLISI mjini Los Angeles wameanzisha uchunguzi dhidi ya Sylvester Stallone  ambaye anatuhumiwa kumbaka mwanamama mmoja miaka 27 iliyopita.
Hata hivyo muigizaji huyo wa sinema za Rambo amesema kwamba madai hayo ni ya kupikwa na kwamba anapanga kumshtaki mwanamke huyo kwa kumsingizia.
Webu ya habari za mastaa ya TMZ imeandika Jumatano wiki hii kwamba  Polisi wa Santa Monica wameanza uchunguzi dhidi ya tuhuma  zilizofikishwa kwao kwa tukio ambalo linadaiwa kufanyika miaka ya 1990.
Wakili wa Stallone, anayetambuliwa kwa jina la Martin Singer alikiri kwamba mwanamke mmoja amepeleka tuhuma kwa tukio ambalo amedai limefanyika miaka 27 iliyopita.
“Mteja wangu anakanusha tuhuma hizo,”  alisema Singer katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.Aidha alisema kwamba Stallone anapanga kupeleka dai Polisi kwamba  mwanamke huyo alikuwa amewasilisha ripoti za uwongo polisi dhidi yake.
Polisi katka mji wa ufukwe ya California wa Santa Monica wamesema jana alhamisi kwamba walikuwa wanachunguza dai ambalo liliwasilishwa kwao mwezi uliopita dhidi ya mwamba huyo ambaye pia anatambulika  katika sinema za “Rocky” .
“Tuliletea dai Novemba mwaka jana la ubakaji tukio lililofanyika katika miaka ya 1990s,” alisema msemaji wa Polisi wa Santa Monica , Saul Rodriguez akizungumza kwa njia ya simu na kuongeza kwamba watakusanya taarifa na chochote ambacho watakipata watakiwakilisha kwa mwendesha mashtaka kufanyia maamuzi.
Kwa mujibu wa sharia za California masuala ya ubakaji yanatakiwa kufanyiwa kazi ndani ya kipindi cha miaka 10 ya tukio lenyewe.
Stallone ambaye kwa sasa ana miaka 71, alipata umashuhuri mwaka 1976 wakati alipocheza sinema iliyopata tuzo ya Oscar ya Rocky na kujipatia sifa za muigizaji mzuri wa sinema za aksheni wakati alipoigiza Rambo.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO