WAZEE  280  wa kituo cha Sakila Hope for Elderly wamepatiwa zawadi ya Christmasi na Wafanyakazi  wa Kampuni ya Tanzania Cigarate Company  (TCC)   yenye thamani  ya Sh, milioni  10.
Wafanyakazi hao wametumia fedha hizo kuwanunulia Wazee hao,  vyakula ,nguo na kuwakabidhi  zawadi hizo, katika hicho, kilichopo  Kata ya Kikatiti , Wilaya ya Arumeru.
Mratibu wa Kituo cha Sakila Hope for Elderly, Humphery Mafie akitoa shukurani kwa niaba ya wazee hao ,alisema hayo jana na kusisitiza kuwa ,wafanyakazi hao ni mfano wa kuigwa na kutaka watu wengine kujitokeza kusaidia wazee hao ,kwa kuwa ni baraka kuwasaidia makundi hayo.
Mafie alisema kuwa  wanakazi kubwa ya kuwatunza na kuwapatia mahitaji wazee hao na kudai kuwa ipo haja ya jamii nzima kushiriki kuwapatia msaada ili waweze kuendelea kuishi   kuwa siyo kazi rahisi kutunza kundi hilo kwa kuwa wana mahitaji mengi ikiwa ni  pamoja na kuwajengea nyumba za kuishi katika makazi yao .
Aidha anasema wanao wazee zaidi ya 10 wanaoishi kambini na kuomba jamii kujitokeza kuwasaidia ili waaendelea kuishi na kusaidia jamii zao kwa kuwashauri kwa kuzingatia ukweli kuwa wazee ni hazina
 Mchungaji Joseph Urio  wa kanisa la Evangalism International ,Ngyeku,akielezea huduma hiyo alisema kuwa watu wengi wamekuwa wabinafsi na familia zao na  kusahau wazee na  kushindwa hata kuwapatia  chakula na kudai kuwa kitendo hicho ni kibaya.
Mchungaji Urio alifafanua kuwa baadhi ya wazee wana watoto wao wenye uwezo wa kuwatunza lakini wamekuwa wabinafsi na hawataki kusikia kuhusu jambo la kuwatunza wazazi wao.
Wazee wanaotunzwa katika kituo hicho wanatoa simulizi na kudai kuwa wana matumaini ya kuishi  maisha marefu kwa msaada wa vyakula na mavazi wanayopata kutoka kutoka kwa watu wenye mapenzi mema na Kitu hicho.
 Source:HabariLeo

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO