MWANAMKE mmoja nchini Pakistan amekamatwa kwa tuhuma za kusababisha vifo vya watu 15 baada ya jaribio lake la kumuua mume kwa sumu kushindwa.
Mwanamke huyo ambaye hakufurahishwa na ndoa yake ya lazima alimtilia sumu mumewe katika maziwa ambayomume alikataa kuyanywa.
Aidha mama mkwe baada ya kuona kwamba kuna maziwa hayakunyweka alitumia kutengeneza kinywaji kinachotumia mtindi kwa ajili ya familia ya watu 27.
Mwanamke huyo wa Punjab, Aasia Bibi, 21, alilazmishwa kuolewa na Amjad Akram. Miezi miwili baada ya ndoa hiyo alitengeneza mpango wa kumuua mume wake.
Sumu aliyoitumia alipewa na  mpenzi wake Shahid Lashari.
Imeelezwa kuwa baada ya kuolewa  na kujikuta hana furaha alirejea nyumbani na kuwaeleza watu wake kwamba hapendi ndoa hiyo lakini wlaimtimua na kurejea kwa mume wake ambako alipanga kumuua.
Alimtengea maziwa Amjad rambaye aliyakataa na baadae glasi hiyo ya maziwa ilionwa na mama mkwe ambaye bila kujua alitumia kutengeneza kinywaji cha Lassi, kinywaji cha asili kilicho maarufu sana katika bara Hindia.
Kinywaji hcho kilitumiwa na familia  ya watu 27 wa Amjad ambao mara tu walionesha dalili za kunywa kinywaji chenye sumu.
Afisa mwandamizi wa polisi amesema kwamba mwanamke huyo alikiri kuweka sumu hiyo akiwa rumande ingawa awali alisema kwamba mjusi alikuwa ameingia katika maziwa hayo na kuyafanya kuwa na sumu.
Imeelezwa kuwa pamoja na Aasia wengine waliokamatwa ni mpenzi wake huyo ambaye alikuwa anataka kuolewa naye na shangazi yake.
Hata hivyo mwanamke huyo alikataa maelezo hayo wakati tuhuma dhidi yake zilipozungumzwa mbele ya  waandishi wa habari.
 “Shahid aliniambia nitie sumu jkatika kinywaji, sikufanya hivyo.Alitaka anioe, nilimkatalia.”

Ingawa Pakistan imeimarisha sheria dhidi ya ndoa za utoto nba dhidi ya kulaizmisha ndoa imekuwa haina la kufanya na wengi wanaokumbana na matatizo hayo huamua maamuzi magumu ya kuangamioza maisha.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO