Episode
1 The Guardian Limited
‘Kaka
Beda’
‘Ndio
Athumani’
‘Nipo
na mtu anayekufahamu, anataka kuzungumza nawe’
‘Nipe”
Niliposikia sauti nilisema: Shikamoo Kanali
Kikwete.
Akacheka
kidogo akajibu marahaba na kuniambia Mtumba (mjomba) bado sijapata hicho cheo
mimi bado Luteni kanali, kauli yako iwe na heri.. nikacheka… ikasema
inshallah..
Nilikuwa
sijaongea na Jakaya Mrisho Kikwete kwa
muda na wakati huo alikuwa wizara ya mambo ya nje na alikuwa anapiga zile za
chini kwa chini kuwajua watanzania kabla hajaomba ridhaa. Kuona atawatumikiaje.
Tulizungumza
nikamwelewa kisha nikamwambia: nipe kaka Athumani.
“Nambie
plani yako”
Aliniambia,
njikamwambia tupo pamoja.
EPISODE
2 HabariLeo
Alikuwa
ameninunulia chakula na tulikuwa tunazungumza:
“kaka
tumezungumza nengi lakinji nadhani tengeneza historia. Tengeneza kitabu cha
hekaheka za uchaguzi. Usiandike kitu. Mapicha tu uliyoyatandika kuanzia chini
kwa chini mnatafuta kuijua Tanzania na watu wake hadi kwenye official kampeni
na Ikulu picha zaidi ya 500 zitakuwa
zimeweka kumbukumbu nzuri sana mkabidhi bwana mkubwa aje kuweka katika maktaba
yake.”
“Hii Makamba anaijua”
“fanyeni
kabla hujapoteza picha hizo kwa namna yoyote ile.”
Tulizungumza
tukakubaliana kwamba atafanya kazi hiyo.
EPISODE 3
HabariLeo
Kaka
mbona umefanya vurugu hapa.
Wala
sijafanya vurugu, hii ni mipango yako. Mimi natekeleza ulichoagiza au
nimekosea?
“picha
mbona umeziondoa nyingine?’
“Zilkuwa
na ukakasi kaka na wewe unanielewa. Tusigombane na mwenye mali”
“kama
hivyo nikuletee nyingine hizi si sawa”
“Poa
hazijaenda mtamboni zilete tu”
Alizileta
na kisha akaniambia kaka naenda kidogo huko
Kusini fasta tu na kurudi”
“Si
unajua ratiba yako kaka?”
“Nakwenda
na gari yangu nafanyakazi na kurejea”
“Poa”
“lakini
vipi safari yako ya masomo?
“nikirudi
tutaongea Chifu.
Poa
EPISODE
4HabariLeo
Kaka Athumani
amepata ajali?
Wapi?
Akasema.
Eneo hilo
si ndilo lile lenye changarawe ?
Ndio
Nikakumbuka:
Eneo hilo siku tano zilizopita tulicheza dansi ya mwaka tukiwa na Toyota ya wizara ya kilimo tukitokea Songea,
kama si umakini wa dereva ilikuwa taabu kidogo gari ilivutwa ikaserereka.
Hapakuwepo na Kibao cha kuonya kwamba unaingia eneo la changarawe.
Hali yake
ikoje?
Hamsini
hamsini
Tukaachana
nikaingia ofisi ya Mhariri Malima.
Kuna tatizo safari ya Athumani na paper zake
hizi hapa. Nikamwachia makaratasi yake pale. Nikaendelea na utaratibu wangu.
EPISODE 5
HabariLeo
Kaka
tumefanikiwa kuishi lakini nina vyuma kibao hapa.
Wewe ni
alama ya ushujaa.
Itakuwaje
yale mambo?
Itategemea
ninavyopona.
Nikawa
namwangalia maendeleo yake, nikiwa hopeless kabisa. Lakini nilikuwa na cha
kujifunza na kujiambia Moyoni Athumani Duhh? Hii hakika ni alama ya utulivu, unahitaji kutulia kweli
kuwa na tabasamu daima pamoja na maumivu yote.
UKURASA
UMEFUNGWA
Leo
asubuhi, mtu anayenifahamu mimi akanipigia simu kunieleza kadhia iliyopo. Na
baadae kaka yangu Rehani akanipigia simu akitaka nithibitishe. Nikamwambia nipo
likizo lakini ni kweli Athumani Hamisi amefariki dunia leo.
EPISODE
SIX
Na
Tumshukuru Mungu kwa Kila kitu, Athumani Mungu na akupe matarajio yako kwa kadri
ya imani yako. Rest in Peace Broo
Post a Comment
Post a Comment