Mwanamtandao moja ambaye alikuwa katika moja ya fukwe ya Nigeria alipata mshtuko mkubwa wakati alipoona chupa mbili zilizofungwa pamoja ambayo moja ilikuwa ndani imetumbukizwa picha ya mtu.
Mwanamtandao huyo aliposti katika akaunti yake ya FB chupa hizo na kuandika maneno ambayo yanavuta hisia kubwa.
Alisema mioyo ya binadamu imekuwa miovu akikariri maandiko katika Biblia.
Mwanamtandao huyo  Keneci Taylor alisema kwamba alipata mshtuko mkubwa na kutokana na simulizi za watu inaonekana aliyefungiwa picha hiyo ndani, ameondolewa uwezo wote wa kuwa na neema na watu wenye hila mbaya za kichawi.
Taylor katika akaunti yake pia alionesha chupa hizo  zilizofungwa pamoja na picha ya mtu ambaye hajatambulika.
Anaandika  hivi: “This is how some people are wicked look what wash out of the beach water on land people be careful of some of them people here”
Uchunguzi wa NAIJ.com unaonesha kwamba kuna njia za giza zinazotumika kuzuia ridhiki za watu au kuwafanyia mambo yanayowafanya wafanye maamuzi ambayo si ya kwao.
Kwa mujkibu wa uchunguzi huo, picha ya mtu huyo asiyejulikana imefanyiwa kafara la kumharibia mambo yake.
Lakini imeelezwa kuwa kitendo cha chupa hizo kufika nchi kavu huenda Mungu ana makusudio ya kumrejeshea ustawi mtu huyo.

Post a Comment

Find Us On Facebook

TANGAZA NASI LEO