MPINA ATAKA KUHAKIKI USHURU WA MIAKA MITANO KATIKA MASOMO YA SAMAKI YA KIMATAIFA

Mkuu wa Wilaya ya Chato   Shabani   Ntarambe (aliyesimama) akimweleza jambo Waziri wa Mifugo na Uvuvi,  Luhaga Mpina(mwenye k...







Mkuu wa Wilaya ya Chato  Shabani  Ntarambe (aliyesimama) akimweleza jambo Waziri wa Mifugo na Uvuvi,  Luhaga Mpina(mwenye kofia) wakati wa mkutano wa hadhara kwenye soko la kimataifa la samaki la Kasenda wilayani Chato leo, ambapo Waziri ameamuru kufanyika ukaguzi mpya wa hesabu za fedha kwenye masoko yote ya kimataifa ya samaki na mazao yake yaliyoko katika Ziwa Victoria ili kuhakiki uhalali wa mapato ya Serikali yaliyokusanywa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.Kulia ni Diwani  wa kata ya Kasenda Muganza Mwita. (Picha  na John Mapepele)





Waziri wa Mifugo na Uvuvi,  Luhaga Mpina(mwenye kofia katikati) akiwa kwenye moja ya boti inayotumika kwa Uvuvi wa samaki kwenye soko la kimataifa la samaki la Kasenda wilayani Chato leo, Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chato Bathromeo Christiani, Kushoto ni Diwani  wa kata ya Kasenda Muganza Mwita. (Picha  na John Mapepele)





Waziri wa Mifugo na Uvuvi,  Luhaga Mpina(mwenye kofia) akiwahutubia wananchi kwenye soko la kimataifa la samaki la Kasenda wilayani Chato leo, ameamuru kufanyika ukaguzi mpya wa hesabu za fedha kwenye masoko yote ya kimataifa ya samaki na mazao yake yaliyoko katika Ziwa Victoria ili kuhakiki uhalali wa mapato ya Serikali yaliyokusanywa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. (Picha  na John Mapepele)







Waziri wa Mifugo na Uvuvi,  Luhaga Mpina(mwenye kofia) akikagua ofisi za soko la kimataifa la samaki la Kasenda wilayani Chato leo, Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi bi Mwanaidi Mlolwa. Nyumba niYohana Mikumbe Mtekinolojia wa samaki katika soko la Kasenda. . (Picha  na John Mapepele)



Umati wa wananchi waliohudhuria mkutano wa Waziri Luhaga Mpina  kwenye soko la kimataifa la samaki la Kasenda wilayani Chato leo, ameamuru kufanyika ukaguzi mpya wa hesabu za fedha kwenye masoko yote ya kimataifa ya samaki na mazao yake yaliyoko katika Ziwa Victoria ili kuhakiki uhalali wa mapato ya Serikali yaliyokusanywa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. (Picha  na John Mapepele)
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi,  Luhaga Mpina ameamuru kufanyika ukaguzi mpya wa hesabu za fedha kwenye masoko yote ya kimataifa ya samaki na mazao yake yaliyoko katika Ziwa Victoria ili kuhakiki uhalali wa mapato ya Serikali yaliyokusanywa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Masoko hayo yatakayohusika na ukaguzi huo ni pamoja na Kirumba Mwanza,  Nyakalilo Buchosa Mwanza ,Kasenda Chato Geita, Magalini Muleba Kagera, Kemondo Bukoba Kagera na Mwigobero Musoma Mara ambapo wafanyabiashara watakaobainika walihusika kufanya udanganyifu wa mapato watatakiwa kurejesha fedha hizo walizoiibia Serikali kwa kipindi hicho ambapo Watumishi wa Umma nao waliohusika kuhujumu mapato hayo watasakwa popote walipo na kufikishwa kwenye vyombo vya dola kukabiliana na mashtaka ya kuhujumu wa rasimali za nchi .
Hatua hiyo ya Waziri Mpina imekuja kufuatia kubaini kuwepo udanganyifu mkubwa katika biashara ya samaki, dagaa,mabondo, na mapanki akibainisha kuwepo tabia ya kupunguza uzito na idadi ya magunia,kubadilisha matumizi ya vibali,kuchanganya mizigo ya ndani na nje ya nchi kwenye malori, kuanzishwa kwa masoko ya kimataifa yasiyo rasmi na wafanyabiashara wakubwa wa mazao ya uvuvi kutolipa kodi za mapato kutoka TRA.
Pia Waziri Mpina ameamuru kufutwa kwa masoko yote yasiyo rasmi yaliyopewa hadhi ya kimataifa ikiwemo soko la Nyakalilo na Magalini ambapo amemuagiza Katibu Mkuu Uvuvi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Yohana Budeba kuwaondoa na kuwapangia vituo vingine vya kazi watumishi waliokuwepo kwenye masoko hayo.
Waziri Mpina ametolea mfano udanganyifu mkubwa uliofanywa na wafanyabiashara na watumishi wa umma wasio waaminifu likiwemo tukio la Disemba 16 mwaka jana ambapo mfanyabiashara mmoja (jina tunalo)huku akitumia gari lenye usajili ya nchi ya Rwanda lenye namba za usajili RB 9591 alipewa kibali cha kusafirisha magunia 258 kwenda Ngara mkoani Kagera na badala yake aliyapeleka nchini Rwanda na kuisababishia Serikali hasara ya sh. Milioni 3.
Pia kupunguza uzito na idadi ya magunia ili kulipia kidogo mapato ya Serikali akitolea mfano mfanyabiashara mwingine (jina tunalo) ambapo Disemba 2 , 2017 kutoka soko la Kasenda alisafirisha magunia 300 ya dagaa lakini yaliyolipiwa mrabaha wa Serikali ni magunia 200 tu huku Serikali ikipoteza mapato ya magunia 100 .
Waziri Mpina amesema matukio hayo ya udanganyifu aliyotolea mfano ni ya siku moja tu huku wafanyabiashara hao wakiwa na utamaduni wa kusafirisha zaidi ya safari nane kwa mwezi ambapo Serikali hupoteza mabilioni ya fedha za mapato kwa mwaka ambapo Samaki, dagaa, kayabo, mabondo, mapanki,furu wamekuwa wakiroroshwa kupitia mipakani na njia ya panya kwenda nchi za Rwanda, Burundi, DRC, Zambia, Malawi, Uganda na Kenya.
Amesema wafanyabiashara waliopewa leseni za kusafirisha mazao ya uvuvi nje ya nchi wamekuwa mawakala wa raia wa kigeni ambapo kazi ya kununua, kukusanya na kusafirisha hufanywa na wageni jambo ambalo ni kinyume cha Sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2009 kifungu cha 13 (14).
Kuhusu kasi ya Uvuvi haramu katika Wilaya ya Chato Waziri Mpina amesema taarifa zinaonesha kwa kipindi cha Januari  hadi Disemba mwaka 2017 zana haramu zikiwemo Timba, Kokoro,Katuri,Mitumbwi, yenye thamani ya sh milioni 525,207,000 vilikamatwa, kutaifishwa na  kuteketezwa.
Ametumia nafasi hiyo kuwasihi wananchi kuacha uvuvi haramu huku akieleza kusikitishwa na namna watanzania hao wazawa walivyopoteza mitaji yao lakini akatangaza msimamo mzito.
“Nimesononeshwa sana na taarifa ya kuteketezwa kwa mitaji ya wafanyabiashara hao wazawa kwa sababu ya kujihusisha na uvuvi haramu lakini nataka kuwakikishia kuwa vita dhidi ya uvuvi haramu haina suluhu na kwamba sitamuonea haya wala huruma mtu yoyote atakayejihusisha na uvuvi haramu tutawashughulikia wote bila huruma kwani Serikali ya awamu ya tano imejidhatiti kukabiliana na uvuvi haramu kwa nguvu zote na bila kuchoka”alisema.
Kwa upande wake Kaimu  Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Uvuvi  wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mwanaidi Mlolwa alisema jukumu la kulinda rasilimali za nchi liko kikatiba  hivyo kila mwananchi ana wajibu wa kusaidia kulinda rasilimali hizo zisitoroshwe kwa manufaa ya nchi ya nyingine.
Amesema Sheria  ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 kifungu cha 37(a) (ii) na (iii) na kanuni zake za mwaka 2009 zinawapa mamlaka wasimamizi wa Sheria hiyo kumkamata mtu yeyote anayekutwa na samaki na mazao yake waliovuliwa kwa njia haramu na kutaifisha mali zote ikiwemo samaki, boti, mitumbwi na magari yaliyobeba samaki hao.
Mkuu wa Wilaya ya Chato, Shabani Ntarambe amesema katika kukabiliana na uvuvi haramu wilaya  kwa kipindi cha Januari  hadi Disemba mwaka 2017 imefanikiwa kukamata ,kutaifisha na kuteketeza zana haramu za uvuvi zikiwemo Timba, Kokoro,Katuri,Mitumbwi, yenye thamani ya sh. milioni 525.2 na kumhakikishia Waziri Mpina kuwa mapambano bado yanaendelea kukomesha kabisa uvuvi haramu

COMMENTS

Name

Anga,11,Arusha,27,Burudani,301,burundani,1,come rain,1,come sun,1,Crazy in Love kama wimbo kama wao wenyewe,1,dahh sijui kweli mbona shida,1,Dar utakuja je tumejiandaa,1,daraja sahau nini,1,demokrasia ya upanga,1,Dodoma,77,Dole tupu vijana wa zamani,1,Duhh bibie endeleza libeneke,1,Duhh kaisikie Walibana,1,duhh kwa mbagala mama lazima awe supa,1,Fedha za maiti haziliwi bure,1,Fedha za watu kwa maendeleo ya watu,1,Fikira,14,filamu,238,Filamu ndio kielelezo cha ukuzi wa taifa,1,flamu,7,Gandamiza Kibara baba ake,1,Habari,4810,habari. dodoma,23,hadithi,19,hakika tumeweka historia,1,hakuna noma jongwe,1,hapa kwetu inakuwaje vile,1,hasira hasara,1,hata maji,1,hataki masikhara na maisha yake,1,hatubonyezi kizenji,1,haya ndiyo mambo ya Ulaya,1,haya si yangu ni ya mdau mwenye hasira,1,haya wabongo na mambo kutoka nje,1,He he he wananikumbusha upishi wa shaba,1,Headline,1,Hii hurejesha uhai,1,Hii iko sawa kweli?,1,Hii imekaa vizuri,1,Hii inakaaje vile,1,Hii kweli noma,1,Hii maana yake Moro kuna uhaba wa chakula,1,Hii mexico,1,Hii mihasira mingine bwana,1,Hii ndio moro sio mpaka dar,1,hii ni hatari,1,Hii ni kiboko anayetaka kubisha ajibishie tu,1,Hii ni moja ya staili za kunyoa nywele,1,Hii si lukwangule,1,hii staili mpya,1,hili ni jengo pacha la malaysia ghorofa 88,1,Hivi ni ngoma tu,1,hivi nini siri za serikali,1,hivi sisi tunajua kama kuna vitu vya aina hii,1,hivi vitu bwana,1,Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia,1,Hizi imani nyingine ni hatari,1,Hizi takwimu hizi mhh,1,Hongera bibie,1,Hongera dada etu kwa kutuletea kaka etu (shemeji) kwani mwenye dada hakosi shemeji,1,Hongera sana,1,huhitaji mifedha kuwa msafi,1,Huko Ulaya,1,Huu ndio ustaarabu,1,huu ujiko utakuwa mkubwa,1,imetosha,1,Inahitaji nidhamu fulani,1,inakuuma au...,1,Inakuwaje kama filamu yenyewe itahitaji busu la nguvu,1,Inaonekana watanzania hatukuwepo,1,Ipo kazi Maximo,1,Iringa,22,Isiwe mijineno tu manake mihela hubadili watu kweli,1,Itakuwa laki moja ya halali,1,jamani huu kama si ushamba kumbe nini,1,Jamani mbona Mungu anatupigania,1,Jamani watoto wanatakiwa kupendwa,1,jamani.. jamani ukiikosa Diamond usijutie,1,Je nyumbani hakuna vitu vya aina hii?Tuambie,1,je walikuwepo watu wa huduma ya kwanza,1,Je watanzania wanalipa kodi,1,jela kwa raha,1,Jolie,1,juhudi za lazima kuinua filamu,1,kama si kiwanda cha chumvi nani atawajua hawa,1,Kama kweli ndio kweli basi kila heri,1,Kama Mkristo naamini hilo hiyo si sahihi,1,kama unajua kuyarudi nenda Malta,1,kama wao wanaweza sisi je,1,Kamua baba waache wakanyagane,1,karibu nyumbani dada yote maisha tu,1,karibu Tatiii,1,KARIBUNI,1,Katavi,5,kaza buti hakuna kukata tamaa inalipa,1,kazi kwako mheshimiwa waziri wa madini,1,kazi na burudani,1,keep it up bloggers,1,kero ya usafiri sasa kwisha,1,Kila chenye roho na mwili kitaonja umauti,1,kila kitu kina vitu,1,Kila la Heri jamila,1,kila la heri kwani ni changamoto,1,Kipya,51,Kiuno bila mfupa,1,Kolelo mzimu ambao bado hai,1,KUBWA,1,Kudumisha urafiki wa dunia,1,Kuna dalili za wasomi kukubali Uafrika,1,kuna makala humu humu ndani ya blogu sijui mnasemaje,1,Kuu,113,kwa mara nyingine tena Tigo imewezesha,1,Kwa mchanganyiko huu muungano lazima udumu,1,Kwa mihasira hajambo,1,kweli,1,Kweli ina mkono mrefu tuone,1,Kweli duniani tunatofautiana,1,la maana ni kuwa na jiko au vipi,1,labda halitabadilika tena,1,lakini mwafaka lazima,1,lengo ni kutafakari,1,leteni vitu tuvione,1,lets us,1,Lucy wanakuelewa hawa...,1,Lukwangule nyumbani kwetu,2,M ungu bariki mikono ya madaktari wafanikiwe,1,MAARUFU,1,maendeleo ya soka siku zote yanahitaji fedha ili yapatikane,1,maisha ni vyema kuyaangalia,1,MAJIBU,1,makala,51,mama ni mama tu anapendeza,1,mambo mengine we angalia tu,1,mambo msimamo,1,mambo sasa mchanganyiko,1,Mara nyingine huona tunakotoka kwa kuona wenzetu,1,Mashabiki wa rhumba mpooooooooo,1,Masitaa,12,Maskani,1,MASOKO,3,Masupa staa mnaoinukia mpoo,1,Matamasha,6,mavazi ya kuogelea yanaposhindaniwa,1,Mbeya,11,Mchakamchaka anti Asmah,1,Mchanganyiko,81,MCHANYATO,1,mchezo,5,mengi wanayoyaita siri ni public information,1,mfumuko wa bei mpaka noma,1,Mhh sijui watu wa Sua ambao wako huko wanasemaje,1,Mhh ugua pole dada watu wanataka burudani,1,Michezo,501,Michezo maalum inatakiwa kupigiwa debe,1,miguu,1,miguu babu,1,Mikataba mingine ama hakika tuiangalie hata wakopeshaji nao wanatugeuza sakala,1,MIMI NI KISURA NAJITAMBUA,1,Mimi sijajua hasa kumetokea nini kwani ninavyojua hawa huwa na ungalizi wa hali ya juu,1,Mimi simo,1,mimi sisemi,1,mkiwa chumvi basi mkoze,1,Mkiwa taa mulikeni,1,Mnaonaje je hii imekaa vyema,1,Mnaweza wakwetu hapa,1,Morogoro,51,mrithi wa mwanadada Whitney Houston,1,Mtwara,4,Mungu aiweke mahali pema roho yake,4,Mungu amrehemu,1,Mungu amweke pema peponi,1,Mungu awabariki sana,1,Mungu awe nao,1,Mungu ibariki Tanzania,1,Mungu tuepushe na imani hizi za kishirikina,1,mungu tufanye tuwe na upendo,1,Mungu twaomba utuhurumie,1,Muziki,350,muziki na fasheni,5,Mwanahabari,33,Mwanza,6,Mwendo mdundo dada,1,Mwenge huo utakimbizwa duniani kwa siku 130,1,Mwenge wa olimpiki ni ishara ya urafiki,1,Mzee wa Farasi nakupa saluti,1,Mzimbabwe huyu kutoka kwa mama mkali,1,N i dar mpaka Moro au bao tatu bila,1,Na sisi je,1,Naam kama haiwezekani hapa,1,Nairobi waanzisha tena utalii,1,namna bora ya kusaidia jamii,1,nani abebe hukumu na lawama,1,nani asiyejua utamu wa pipi,1,Nani kama baba,1,naona inafaa kuchangia mimi sitoi hoja,1,ndoa za mastaa huwa na mgogoro,1,nenda mwaya nenda,1,New Zanzibar Modern Taarab na wapenzi big up,1,news,5,Ni bikini kwa kwenda mbele,1,Ni Dar mpaka Moro au.. tatu bila,1,ni furaha za muungano,1,Ni kazi ngumu yenye kuhifadhi utamaduni,1,Ni kuchakarika kuonyesha urafiki na biashara pia,1,ni mfumuko wa bei au mfumuko wa nchi,1,Ni muhimu kutazama afya yako,1,ni muziki kwa kwenda mbele,1,Ni muziki mpaka China,1,Ni raha tupu,1,Ni Serengeti Premium Lager,1,Ni Tigo na mawasiliano ya kisasa,1,Ni wakati wa kuujadili utamaduni,1,Ni zaidi ya jazz,1,Nitasubiri and welcome home,1,nje je?,1,NUKUU YA LEO,1,nyie mnasemaje kuhusu hili,1,Ona Kolelo na sindikizwa na Wazee wa Gwasuma,1,ona vya dunia,1,One step ahead,1,patna mwingine mjamzito,1,Pengine anamuogopa Jada Pinkett manake kwa wivu..,1,picha,494,Pole Jamila hayo ndiyo mashindano,1,poleni sana,1,poleni sana wanyalukolo,1,Powa sana,1,Profesa jamaa wanakumaindi,1,Roho za marehemu zipate pumziko la milele,1,Ruvuma,9,sakata dansi mpaka kwenye kilele cha dunia,1,sasa kumebakia ugonjwa mmoja polisi kuendesha mashtaka,1,sasa mifedha kila mahali hongereni,1,Sasa ni mavuno,1,Sasa ni wakati wa kutafuta upenyo ndani ya IDOLS,1,SAYANSI,1,SAYANSI ANGA,1,See Uluguru Montains,1,serikali inataka kujihami kwanini,1,Show of support Big Up Madame,1,Si kitu kidogo hata kidogo,1,si unajua tena namie naimwaga hivyo hivyo,1,Siasa,346,siasa habari,2,Sijui kama City wanajua Mbagala noma,1,Sijui tunaishi karne gani yailahi,1,Sinema,9,sio advencha....kaaa ...niko kibaruani,1,Sisi ndio tunaanza vitongoji,1,Sisi yetu macho na masikio,1,Slow slow jamani,1,tabasamu kali la mwenge wa olimpiki,1,Tabora,1,Tazama Waziri Mkuu Pinda wasije wakapindisha maamuzi yako,1,TEKNOLOJIA,1,Thats big man game,1,This is crazy Africa,1,This is Mgeta,1,Tibet wamegeuza Olimpiki jukwaa la siasa,1,Titbits collection,1,Tubadili tamaduni,1,Tuchangie mambo yaive,1,tuendeleze sanaa,1,tuienzi na sisi mbona wizara haituambii,1,Tuipeleke kaskazini,1,Tuisaidie serikali shida ya Mererani,1,tujue namna ya kupumzika,1,Tulienda kustarehe au kufanya fujo,1,Tumsaidie mtototo huyu kurejea katika hali ya kawaida,1,tunahitaji haya,1,Tunajifunza kweli kutoka kwao,1,Tunapandisha chati tu,1,Tunasubiri,1,tunazidi kuhesabu siku,1,TUNAZISUBIRI ZA VINARA ADAR,1,Tuombe nafuu kwa wagonjwa,1,Tuombe rehema kwa mungu,1,Tuone yatufae,1,Tusingoje wengine watusemee,1,tutampa tafu kubwa Prof,1,tuuenzi utamaduni au vipi,1,Tuukuze na kuulinda,1,tuvipende,1,tuwalinde maalbino,1,Tuwe kweli wakweli,1,ubunifu siku zote hulipa,1,uchumi huzunguka kwa kuwawezesha wasukaji,1,udumu muungano,1,Ugonjwa huu wa sasa ni kitendawili,1,Ukiiona kolelo utaipenda,1,Ukirejea salama kila mtu anafurahi,1,Umelenga Mkuchika utamaduni unakufa,1,unaposaka uwakilishi wa dunia,1,urafiki,1,Usisahau wazee wa Ngwasuma,1,UTAMADUNI,1,Video,2,Vionjo vipya ndani ya Gwasuma,1,Vita dhidi ya ufisadi,1,vitongoji Miss Tanzania navyo vimeanza,1,Vitu vikali vyazidi kuingia Dar,1,Vituko,77,Vituo vya polisi Tanga vyatelekezwa,1,VIVALO,1,Wacha tujifue,2,Wadau ilitolewa kiingereza,1,wakali wa ubunifu,1,wala usibabaike mwakwetu hii noma,1,wanadamu wanapotaka kujua zaidi,1,wanasema mpaka kieleweke,1,Wanataka kujua mali za JK na wengine,1,Wanawake wenye mvuto: Monroe,1,Wapo mabinti wa matawi ya juu,1,watu wanapofanya weli kwenye sanaa,1,waweza kurejea enzi ya Moro jazz na Cuban malimba,1,Wazee tupo kusindikiza,1,waziri,1,welcome dar baby,1,Wenzetu wameona sisi tunangoja nini kuangalia,1,wewe unasemaje,1,wigo mpana wa utamaduni,1,wilaya ya 'Mbagala' mlie tu,1,Yaaani sijui itawezekana,1,Yaani wakati mwingine hata huelewi prioty over priority,1,yeye mbele sisi nyuma,1,Yote maisha dada,1,ZA MOTOMOTO,1,Zanzibar,79,zawadi zinatakiwa ziende shule,1,ZILIZOTIA FORA,1,zitachangia kupunguza makali ya bei za umeme,1,
ltr
item
Lukwangule Entertainment: MPINA ATAKA KUHAKIKI USHURU WA MIAKA MITANO KATIKA MASOMO YA SAMAKI YA KIMATAIFA
MPINA ATAKA KUHAKIKI USHURU WA MIAKA MITANO KATIKA MASOMO YA SAMAKI YA KIMATAIFA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg0ZcOq_U55QU-pPCHe6TQpr93IUtm3XsYHNiji3Mmwx2XMXSAsSAyREUGlBnkki1x3Q2EIfDhotOIJaCPHqEvzxYKab9RYNbmIgxTdbm0cPQkA4LX__Q-8L6UnD866D5tmAY99GYY6r93G/s640/a.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg0ZcOq_U55QU-pPCHe6TQpr93IUtm3XsYHNiji3Mmwx2XMXSAsSAyREUGlBnkki1x3Q2EIfDhotOIJaCPHqEvzxYKab9RYNbmIgxTdbm0cPQkA4LX__Q-8L6UnD866D5tmAY99GYY6r93G/s72-c/a.jpg
Lukwangule Entertainment
http://lukwangule.blogspot.com/2018/01/mpina-ataka-kuhakiki-ushuru-wa-miaka.html
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/
http://lukwangule.blogspot.com/2018/01/mpina-ataka-kuhakiki-ushuru-wa-miaka.html
true
934549962738256429
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy